Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa Tanzania haitakubali kulazimishwa kuiga tamaduni za mataifa ya Magharibi, ikiwemo ndoa za jinsia moja, na kusisitiza kuwa CCM itaendelea kuongoza kwa ridhaa ya Watanzania kuepuka mambo hayo.
Akizungumza Januari 29, 2025, katika mkutano wa hadhara mkoani Geita kuelekea Maadhimisho ya Miaka 48 ya CCM, Wasira amesema kuna njama za baadhi ya watu aliowaita ‘vibaraka’ kutaka kupenyeza ajenda za mataifa ya nje, ikiwemo kuhalalisha ndoa za jinsia moja, jambo ambalo CCM haitakubali.
"Wanatumia vibaraka wao, wanataka utamaduni wao utawale mawazo yetu? Mpaka wanafikia mahali wanataka wanaume waoane na wanawake waoane kwa wanawake, hao ndio walio na vibaraka wao ndani ya Tanzania ambao wanasema tumekaa sana, tumewachelewesha wanaume kuoana maana hatukubaliani nao," amesema Wasira.
Aidha, amezungumzia madai kuwa CCM imekaa madarakani muda mrefu na kusema kuwa chama hicho kimeendelea kuleta maendeleo makubwa nchini, ikiwa ni pamoja na kupanua elimu kwa watoto wa Tanzania.
"Tulidai uhuru kwa sababu tulikuwa na ajenda ya maendeleo na mabadiliko ambayo wakoloni walishindwa kuyaleta. Leo tuna mamilioni ya watoto wanasoma, tena tunasomesha watoto wetu wote. Asilimia kubwa ya watoto wa Tanzania wanakwenda shule. Huko Geita walipoondoka hakukuwa na hata sekondari moja, leo zinafikia 90 zilizojengwa ndani ya miaka minne. Ni nani kama Rais Samia Suluhu Hassan?" amehoji Wasira.
Soma, Pia: Wasira: Hatukatai mazungumzo, lakini hatuwezi kuamrishwa, asisitiza sera ya Samia ya 4R
Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kushikilia madaraka kwa kuwa inaungwa mkono na wananchi na si kwa makubaliano na taifa lolote la nje.
"Tunawaambia hatukuwa na mkataba na mtu, tupo hapa kwa idhini ya Watanzania na sisi tutaendelea kuwepo, hatuna mpango wa kutoka madarakani," amesisitiza.