Pre GE2025 Wasira: Mabeberu na Vibaraka wao wanataka kuleta Ushoga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii verse bado ipogo tu? Wanatufanya manyani tu kama kawa
 
"Wanatumia vibaraka wao, wanataka utamaduni wao utawale mawazo yetu? Mpaka wanafikia mahali wanataka wanaume waoane na wanawake waoane kwa wanawake, hao ndio walio na vibaraka wao ndani ya Tanzania ambao wanasema tumekaa sana, tumewachelewesha wanaume kuoana maana hatukubaliani nao," amesema Wasira.
Watamshughulikia asipokuwa makini
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa Tanzania haitakubali kulazimishwa kuiga tamaduni za mataifa ya Magharibi, ikiwemo ndoa za jinsia moja, na kusisitiza kuwa CCM itaendelea kuongoza kwa ridhaa ya Watanzania kuepuka mambo hayo.

Akizungumza Januari 29, 2025, katika mkutano wa hadhara mkoani Geita kuelekea Maadhimisho ya Miaka 48 ya CCM, Wasira amesema kuna njama za baadhi ya watu aliowaita ‘vibaraka’ kutaka kupenyeza ajenda za mataifa ya nje, ikiwemo kuhalalisha ndoa za jinsia moja, jambo ambalo CCM haitakubali.

"Wanatumia vibaraka wao, wanataka utamaduni wao utawale mawazo yetu? Mpaka wanafikia mahali wanataka wanaume waoane na wanawake waoane kwa wanawake, hao ndio walio na vibaraka wao ndani ya Tanzania ambao wanasema tumekaa sana, tumewachelewesha wanaume kuoana maana hatukubaliani nao," amesema Wasira.

Aidha, amezungumzia madai kuwa CCM imekaa madarakani muda mrefu na kusema kuwa chama hicho kimeendelea kuleta maendeleo makubwa nchini, ikiwa ni pamoja na kupanua elimu kwa watoto wa Tanzania.

"Tulidai uhuru kwa sababu tulikuwa na ajenda ya maendeleo na mabadiliko ambayo wakoloni walishindwa kuyaleta. Leo tuna mamilioni ya watoto wanasoma, tena tunasomesha watoto wetu wote. Asilimia kubwa ya watoto wa Tanzania wanakwenda shule. Huko Geita walipoondoka hakukuwa na hata sekondari moja, leo zinafikia 90 zilizojengwa ndani ya miaka minne. Ni nani kama Rais Samia Suluhu Hassan?" amehoji Wasira.

Soma, Pia: Wasira: Hatukatai mazungumzo, lakini hatuwezi kuamrishwa, asisitiza sera ya Samia ya 4R

Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kushikilia madaraka kwa kuwa inaungwa mkono na wananchi na si kwa makubaliano na taifa lolote la nje.

"Tunawaambia hatukuwa na mkataba na mtu, tupo hapa kwa idhini ya Watanzania na sisi tutaendelea kuwepo, hatuna mpango wa kutoka madarakani," amesisitiza.
Picha ya utotoni ya Mzee Wasira
 
Attachments

  • FB_IMG_1738421874362.jpg
    FB_IMG_1738421874362.jpg
    65.4 KB · Views: 2
Mbona hakuna Taifa ambalo sio kibaraka wa Mabeberu ishu ni kwamba hata hao Mabeberu wanashangaa kuona libeberu CCM linafanya kazi kubwa ambayo hata wao wasingeifanya kwa umaridadi huo ndio maana Mabeberu sasa watafanya juu chini CCM ibaki madarakani kwa kuwa ni wafanyanyi kazi nzuri zaidi ya Beberu. Shida sio kubwa kibaraka wa Beberu Tunataka Viongozi na CCM yao waamke kwenye huu ulafi na upofu walio nao kwasababu watanzania sahivi wameanza kuelewa black and white. Uzuri tumbo lililoshiba haliwezi kumtambua mwenye Njaa. Ni muda wa Watanzania na waafrika kuamka na kujipambania sisi wenyewe Walitutawala kwa nguvu tukazinduka wakatutawala na wanatutawala kwa akili ni muda sasa wa kuzinduka lasivo hii ndio itakuwa Destiny yetu mpaka kila mtu anafikia Mwisho wake.
 
Watu wameamua wenyewe kukalia msumari wa nyuma
 
Tujiulize kwa kina hawa chadema na kiongozi wao, NI KIPI KIPYA WANAWEZA KUTULETEA KATIKA TAIFA LETU? /OBVIOUSLY HAKUNA!, ZAIDI YA GHASIA TU.
una mentality duni kunako propaganda. Nani anataka ghasia?
 
Hayo umeyasema wewe, vipi kuhusu mama aliyesema mikopo anayokopa haiendi kushona sare za harusi?

Kwani kamala Harris alipokuja kumtembelea mama waliongea nini?
Hivi Kamala alikuwa anaunga mkono mashogo? Basi ndo maana aloshindwa uchaguzi !!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa Tanzania haitakubali kulazimishwa kuiga tamaduni za mataifa ya Magharibi, ikiwemo ndoa za jinsia moja, na kusisitiza kuwa CCM itaendelea kuongoza kwa ridhaa ya Watanzania kuepuka mambo hayo.

Akizungumza Januari 29, 2025, katika mkutano wa hadhara mkoani Geita kuelekea Maadhimisho ya Miaka 48 ya CCM, Wasira amesema kuna njama za baadhi ya watu aliowaita ‘vibaraka’ kutaka kupenyeza ajenda za mataifa ya nje, ikiwemo kuhalalisha ndoa za jinsia moja, jambo ambalo CCM haitakubali.

"Wanatumia vibaraka wao, wanataka utamaduni wao utawale mawazo yetu? Mpaka wanafikia mahali wanataka wanaume waoane na wanawake waoane kwa wanawake, hao ndio walio na vibaraka wao ndani ya Tanzania ambao wanasema tumekaa sana, tumewachelewesha wanaume kuoana maana hatukubaliani nao," amesema Wasira.

Aidha, amezungumzia madai kuwa CCM imekaa madarakani muda mrefu na kusema kuwa chama hicho kimeendelea kuleta maendeleo makubwa nchini, ikiwa ni pamoja na kupanua elimu kwa watoto wa Tanzania.

"Tulidai uhuru kwa sababu tulikuwa na ajenda ya maendeleo na mabadiliko ambayo wakoloni walishindwa kuyaleta. Leo tuna mamilioni ya watoto wanasoma, tena tunasomesha watoto wetu wote. Asilimia kubwa ya watoto wa Tanzania wanakwenda shule. Huko Geita walipoondoka hakukuwa na hata sekondari moja, leo zinafikia 90 zilizojengwa ndani ya miaka minne. Ni nani kama Rais Samia Suluhu Hassan?" amehoji Wasira.

Soma, Pia: Wasira: Hatukatai mazungumzo, lakini hatuwezi kuamrishwa, asisitiza sera ya Samia ya 4R

Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kushikilia madaraka kwa kuwa inaungwa mkono na wananchi na si kwa makubaliano na taifa lolote la nje.

"Tunawaambia hatukuwa na mkataba na mtu, tupo hapa kwa idhini ya Watanzania na sisi tutaendelea kuwepo, hatuna mpango wa kutoka madarakani," amesisitiza.
Uchaguzi uliopita (tamisemi) kama kuna sehemu ccm ilishinda ni chini ya 20%
 
Back
Top Bottom