PreGE2025 Wasira: Namshangaa Mbunge (Mpina) kusema Jimboni kwake bado wanamdai Rais Samia

PreGE2025 Wasira: Namshangaa Mbunge (Mpina) kusema Jimboni kwake bado wanamdai Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amesema amesikitishwa na mbunge (hamkumtaja jina) aliyesema anamdai Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wenzake hawana deni naye na kwamba mbunge huyo ameingia ‘choo ambacho sio chake.

Soma > Mpina: Rais Samia jimboni Kisesa tunakudai, wanaosema 'hatukudai' fedha zao zihamishiwe Kisesa

Kauli ya Wasira inakuja siku moja tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu (CCM) Luhaga Mpina kuzungumza mbele ya Rais Dk.Samia aliyekuwa ziarani mkoa humo kudai kwamba bado wanamdai Rais, hata hivyo Rais Samia alimwambia mbunge huyo anamshangaa kwa kusema bado anamdai.

Akizungumza na wanachama wa CCM katika kikao cha ndani kilichofanyika leo Juni 18, 2025 Geita Mjini, Makaku Mwenyekiti Wasira alisema amesikitishwa na rafiki yake mmoja (hakumtaja jina) kusema wanamdai Rais Dk. Samia.

“Kwa hiyo nimesikitika rafiki yangu mmoja sitaki kumtaja jina yeye anasema sisi tunakudai anamwambia Rais. Wenzake wanasema miaka uliyokaa (Rais) umefanya mengi na hatuna deni na wewe hawakusema amemaliza matatizo yote akimaliza sasa tunakwenda kuchagua Rais mwingine wa nini simatati hakuna.

“Tunachosema kwa muda tuliokupa na kwa matatizo uliyotatua Rais unastahili kupewa muda zaidi kwa sababu umethibitisha kwamba unao uwezo mkubwa wa kusaidia nchi yetu.”

Akifafanua zaidi Wasira alisema Rais amekaa madarakani na amefanya mengi lakini wako watu wanadhani unaweza kumaliza matatizo yote ndani ya miaka mitano, hao ni watu wa ajabu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Dunia yenyewe vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasema aliumba mbingu na nchi kwa siku sita ya saba akapumzika, sasa kama Mungu anaumba kwa siku sita mpaka anataka likizo itakuwa sisi.

“Sisi tunafanya hatua tunapunguza matatizo au tunaondoa matatizo halafu tunaleta maendeleo na maendeleo yanazaa matatizo mapya hakuna unaweza kusema leo matatizo yote yamekwisha, wewe nawe utakuwa umekwisha lakini sio matatizo yataendelea kuwepo.”

Alifafanua ndio maana Chama Cha Mapinduzi ni chama cha kudumu cha kupambana na matatizo ya kimaendeleo na ingekuwa matatizo yote yanaisha mbona wameandika Ilani na yeye(Wasira) alikuwa mjumbe wa kamati Ilani.

“Najua sitaki ila kuieleza hapa kwa sababu watu wa kuieleza watakuja kutuambia tumefika hatua yetu mpaka hapa, tumefanya vizuri sana lakini bado tuna matatizo na tuna majibu ya matatizo hayo.

“Kwa hiyo huyo anayefikiri kwamba Rais angemaliza matatizo yote na yeye ni mbunge hakuyamaliza yote pale kwake maana yako matatizo ya Rais,matatizo ya wabunge na yako matatizo ya madiwani.”

Alisisitiza na hakuna mtu anayemaliza yote ila tunawashukuru wakifanya mambo mazuri kama tunavyomshukuru rais wetu.Ametumia nafasi hiyo kumshauri yule mbunge tena ni rafiki yake sana ila yeye naye ameingia choo kisichokuwa cha kwake ange 'cheki' vizuri.
 
1749741241323.jpg

Moja ya watu wa hovyo kabisa waliopaswa kutokuiona karne ya 20 kabisa
 
Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, amesema amesikitishwa na mbunge (hamkumtaja jina) aliyesema anamdai Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wenzake hawana deni naye na kwamba mbunge huyo ameingia ‘choo ambacho sio chake.

“Kwa hiyo nimesikitika rafiki yangu mmoja sitaki kumtaja jina yeye anasema sisi tunakudai anamwambia Rais. Wenzake wanasema miaka uliyokaa (Rais) umefanya mengi na hatuna deni na wewe hawakusema amemaliza matatizo yote akimaliza sasa tunakwenda kuchagua Rais mwingine wa nini simatati hakuna.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Tunachosema kwa muda tuliokupa na kwa matatizo uliyotatua Rais unastahili kupewa muda zaidi kwa sababu umethibitisha kwamba unao uwezo mkubwa wa kusaidia nchi yetu.”

kwa hiyo huyu mzee ndiyo kaja kumtetea mama yenu kama kisesa hawamudai?kudaiwa imekua tatizo
 
Huwa najiuliza akili za maccm sijui yakoje wanataka kumpangiavMpina nini cha kusema. #Mpina siyo Mwijaku
 
Huyu alikumbatiq mbuyu akiroga pale St Peters. Mbuyuni
Sasa uchawi umemlipa
 
Ila akili za miccm, sasa ndio kaongea nini🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Pale Korogwe mjini anadaiwa au hadaiwi
Watanganyika wote tunamdai reforms kwenye sheria za uchaguzi ili tuwe na uchaguzi huru na wa haki utakaotupatia viongozi bora wanaotokana na matakwa ya wananchi wenyewe.
 
Wazee wanazeeka na kuwa na hekima na maarifa mengi lakini huyu anazidi kuwa chawa na mjinga
 
Back
Top Bottom