Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Kunazidi kufurukuta, moshi unaongezeka!
====
Wakati kitendo cha kuzuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za nchi hiyo kwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman na mwenzake wa Chadema, Tundu Lissu kukizua mjadala, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amejitosa kwenye sakata hilo.
Wasira amesema kuwa kuzuiwa kwa viongozi hao na mamlaka za nchi za Angola, hawapaswi kutafuta mchawi wala kuinyooshea kidole Serikali ya Tanzania.
Pia soma ACT: Viongozi wetu waliozuiwa kuingia Angola wamerejea Nchini, tunasikitishwa na ukimya wa Serikali ya Tanzania
Akizungumza leo Ijumaa Machi 14, 2025 kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe, wakati akianza ziara yake ya siku tatu mkoani humo, Wasira amesema kila nchi ina utaratibu wake ambao ni lazima uheshimiwe.
"Leo nimesoma kuna viongozi walikuwa wanaenda Angola, lakini wamenyang'anywa hati za kusafiria, huko ni Angola sio Tanzania, hapa hakuna aliyenyang’anywa hati yake na hata ikiisha muda wake tunawapa nyingine ili waende wanakotaka na kurudi salama.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Wanalalamika kwa nini Serikali imekaa kimya sasa kwani, sisi tunasimamia Uwanja wa Ndege wa Angola? Ule uwanja unasimamiwa na watu wa Angola, na huenda walikuwa na jambo ambalo wanalitilia shaka," amesema Wasira na kuongeza: “Sasa kuwaambia tu msiingie nchini kwetu kuna tatizo gani, si mrudi tu nyumbani?
Mwananchi