Pre GE2025 Wasira: Othman, Lissu wasitafute mchawi kuzuiwa kuingia Angola. Serikali haisimamii Uwanja wa Angola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Kunazidi kufurukuta, moshi unaongezeka!

====

Wakati kitendo cha kuzuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za nchi hiyo kwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman na mwenzake wa Chadema, Tundu Lissu kukizua mjadala, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amejitosa kwenye sakata hilo.

Wasira amesema kuwa kuzuiwa kwa viongozi hao na mamlaka za nchi za Angola, hawapaswi kutafuta mchawi wala kuinyooshea kidole Serikali ya Tanzania.

Pia soma ACT: Viongozi wetu waliozuiwa kuingia Angola wamerejea Nchini, tunasikitishwa na ukimya wa Serikali ya Tanzania

Akizungumza leo Ijumaa Machi 14, 2025 kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe, wakati akianza ziara yake ya siku tatu mkoani humo, Wasira amesema kila nchi ina utaratibu wake ambao ni lazima uheshimiwe.

"Leo nimesoma kuna viongozi walikuwa wanaenda Angola, lakini wamenyang'anywa hati za kusafiria, huko ni Angola sio Tanzania, hapa hakuna aliyenyang’anywa hati yake na hata ikiisha muda wake tunawapa nyingine ili waende wanakotaka na kurudi salama.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Wanalalamika kwa nini Serikali imekaa kimya sasa kwani, sisi tunasimamia Uwanja wa Ndege wa Angola? Ule uwanja unasimamiwa na watu wa Angola, na huenda walikuwa na jambo ambalo wanalitilia shaka," amesema Wasira na kuongeza: “Sasa kuwaambia tu msiingie nchini kwetu kuna tatizo gani, si mrudi tu nyumbani?

Mwananchi
Marehemu wasira
 
Waambie hao comrade .. kutwa kujilalamisha tu
 
Eti huenda kuna jambo wanalitilia shaka....anazungumza kama shoga la Tanga
 
na viongozi wa chadema inasemekana wametumia jumla ya milioni 45 za tone tone kwa safari hiyo ya Angola, na utapeli wa kidigitali unaendelea muda huu 🐒
Narudia tena, haichekeshi. 🌈 Unakwama wapi?
 
Kuliko tunavyotapeliwa kwenye michango ya shuruti za mbio za mwenge?
wewe last week zimechangwa milioni 64, milioni 45 zimetumika kwa safari moja tu ya kwenda hapo Angola,

jitu limeng'ang'ana kudhulumiwa kidigitali, kama zuzu vile, dah!🐒
 
  • Kicheko
Reactions: UCD
wewe last week zimechangwa milioni 64, milioni 45 zimetumika kwa safari moja tu ya kwenda hapo Angola,

jitu limeng'ang'ana kudhulumiwa kidigitali, kama zuzu vile, dah!🐒
Mbio za mwenge tumetapeliwa tukiwa wanafunzi wa shule ya msingi hadi na utu uzima huu, itakuwa hiyo tonetone ya wiki 2?
 
sasa gentleman hiyo tone tone ya kutoa huku na kuishia kule si itakufanya uzeeke kwa stress sana?🐒
 
Nizeeke zaidi ya nilivyozeeshwa na michango ya mbio za mwenge tena bila ridhaa yangu?
kwa ridhaa ya waTanzania wote mambo ya kitaifa hufanyika, kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi

hayupo wa kubabaika na msusaji wa wa michakato ya kidemokrasia kama wewe gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom