Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira akizungumza katika mahojiano na TBC leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna njia ya mkato ya kupata amani ya kudumu nchini isipokuwa kwa njia ya mazungumzo. Akizungumza katika yaliyochapishwa na TBC , Wasira amebainisha kuwa maridhiano ya kisiasa hayahitaji fedha bali yanahitaji nia thabiti ya pande husika kukutana na kujadiliana.
Wasira amejibu madai ya baadhi ya wanasiasa wanaopinga uhalali wa serikali iliyopo madarakani kwa kufafanua kuwa uhalali huo unatokana na wananchi waliopiga kura, huku akiongeza kuwa kutoshiriki uchaguzi ni hiyari ya mtu lakini hakuzuii wengine kuendelea na mchakato huo. Amewataka wale wote wenye malalamiko kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kutatua changamoto zilizojitokeza, kabla ya kuhamia kwenye hatua inayofuata ya kujadili Katiba.
"Ukiwasikia rafiki zetu huko wanasema sema barabarani... wanasema mambo mengi sana, mengine si mazuri sana lakini unayavumilia. Eh, umesikia wanasema sisi siyo serikali halali.
Sasa ukienda kugombana nao, unagombana nao kuhusu nini? Maana uhalali sisi tunajua upo, maana uhalali unatokana na wananchi. Kuna wenzetu hawakutaka kupiga kura wala kugombea, na hakuna sheria inayowalazimisha. Lakini ukikataa kugombea, huzuia wanaotaka kugombea wakagombea"-Amesema Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira