Wasira: Serikali yetu ni halali kwa sababu imechaguliwa na wananchi

Wasira: Serikali yetu ni halali kwa sababu imechaguliwa na wananchi

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira akizungumza katika mahojiano na TBC leo


​

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna njia ya mkato ya kupata amani ya kudumu nchini isipokuwa kwa njia ya mazungumzo. Akizungumza katika yaliyochapishwa na TBC , Wasira amebainisha kuwa maridhiano ya kisiasa hayahitaji fedha bali yanahitaji nia thabiti ya pande husika kukutana na kujadiliana.

Wasira amejibu madai ya baadhi ya wanasiasa wanaopinga uhalali wa serikali iliyopo madarakani kwa kufafanua kuwa uhalali huo unatokana na wananchi waliopiga kura, huku akiongeza kuwa kutoshiriki uchaguzi ni hiyari ya mtu lakini hakuzuii wengine kuendelea na mchakato huo. Amewataka wale wote wenye malalamiko kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kutatua changamoto zilizojitokeza, kabla ya kuhamia kwenye hatua inayofuata ya kujadili Katiba.

"Ukiwasikia rafiki zetu huko wanasema sema barabarani... wanasema mambo mengi sana, mengine si mazuri sana lakini unayavumilia. Eh, umesikia wanasema sisi siyo serikali halali.

Sasa ukienda kugombana nao, unagombana nao kuhusu nini? Maana uhalali sisi tunajua upo, maana uhalali unatokana na wananchi. Kuna wenzetu hawakutaka kupiga kura wala kugombea, na hakuna sheria inayowalazimisha. Lakini ukikataa kugombea, huzuia wanaotaka kugombea wakagombea"-Amesema Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira
 
IMG-20260714-WA0007.jpg
 
Kama ingekuwa halali kusimgekuwa na agenda za halali au si halali

Ni nani kakuuliza swali Hilo kama si kwamba unajua fika kwamba KWELI si halali..?
 
Ilichaguliwa na wananchi wapi?
Lini
Na saa ngapi?
Mm binafsi nilijiandikisha kituo Cha minazi mirefu kurasini pr. Sikwenda kabisa kupiga kura baada ya machafuko nikaenda na nikagundua nilipigiwa kura!
Chama Cha CHauma kilipata kura lakini 2 ambayo ni chini ya 5% ya kura zote lakini kina wabunge wawili wa viti maalumu bungeni how?
Wasira huhitaji kusimama mbele za watu. na kusema mm ni halali kwa sababu nalala na mama yenu. Yapaswa watoto wakutambue
 
Ilichaguliwa na wananchi wapi?
Lini
Na saa ngapi?
Mm binafsi nilijiandikisha kituo Cha minazi mirefu kurasini pr. Sikwenda kabisa kupiga kura baada ya machafuko nikaenda na nikagundua nilipigiwa kura!
Chama Cha CHauma kilipata kura lakini 2 ambayo ni chini ya 5% ya kura zote lakini kina wabunge wawili wa viti maalumu bungeni how?
Wasira huhitaji kusimama mbele za watu. na kusema mm ni halali kwa sababu nalala na mama yenu. Yapaswa watoto wakutambue
Gentleman,
Serikali sikivu ya CCM,
ni serikali ya waTanzania wote, kwasababu ilipewa dhamana na umma wa waTanzania kushika dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea waTanzania wote maendeleo endelevu ya kiuchumi, kisiasa na kiuchumi.

Iko hivyo tangu oct.2025,
itaendelea kua hivyo kwa mujibu wa katiba, na bila shaka yoyote ile, Oct.2030, waTanzania wote wataipatia tena CCM dhamana na fursa ya kuunda serikali, kuwatumikia wananchi na kuwalinda waTanzania wote dhidi ya vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ambao kumbe ndio adui mkubwa sana wa amani, umoja na usalama wa taifa letu.


So,
makamu mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Stephen Masatu Wasira, yupo sahihi 100%.

wajulishe na wenzako kuhusu hili bila kificho, na itapendeza zaidi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom