Wasira: Siachii ubunge kwa vijana ni wavuta bangi..!!!

Wasira: Siachii ubunge kwa vijana ni wavuta bangi..!!!

yule mwanae wa Chi town anakula musuba kwa kwenda mbele
 
Politically bankrupt!!! Kwani kuvuta bangi kuna uhusiano gani na ubunge au busara kwa jumla? Hajui kuwa hata marais wa marekani akina Clinton, Bush na Obama walishavuta bangi?

- Mwalimu vipi tena hapo? Yaaani Tanzania tuhalalishe kua na viongozi wavuta bangi kwa sababu marais wa US waliwahi kuwa wateja wa bangi? Eti kuna kiongozi anayevuta bangi na bado ana busara ya kuwaongoza wananchi? Wapi huko na ni nani huyo?

- Yaani sasa Great Thinkers tunaanza ku-endorse wavuta bangi bungeni? Hii hoja ya Waziri Wassira mbona kama ni nzito na ni valid. Halafu vipi hoja ya Waziri ikijibiwa kwa hoja, badala ya viroja?

Respect.

FMEs!
 
Nadhani swala la msingi ni watanzania wenyewe wanaopiga kura na wala sio umri au gender ya mtu anayegombea uongozi. Kama waTanzania wanaona mtu wa miaka 70 ndiye anayefaa kuwaongoza na anawaletea maendeleo wanayohitaji, then sio vibaya huyo mtu akichaguliwa. Pia wapo vijana ambao wameingia bungeni na kupata nafasi za uongozi lakini rekodi yao inadhihirisha kwamba ni watu wa hovyo na hawafai, kwa hiyo sidhani kulijaza bunge na vijana ndiyo solution ya matatizo yetu.

Solution ya matatizo yetu ni pale waTanzania watakapo amka kutoka usingizi waliomo na kuamua kuchagua viongozi waadilifu na wazalendo na sio kuchagua watu kwa sababu ya fedha au kwa kufuata upepo, hasa watu wanaosimamishwa na CCM.
 
- Mwalimu vipi tena hapo? Yaaani Tanzania tuhalalishe kua na viongozi wavuta bangi kwa sababu marais wa US waliwahi kuwa wateja wa bangi? Eti kuna kiongozi anayevuta bangi na bado ana busara ya kuwaongoza wananchi? Wapi huko na ni nani huyo?

- Yaani sasa Great Thinkers tunaanza ku-endorse wavuta bangi bungeni? Hii hoja ya Waziri Wassira mbona kama ni nzito na ni valid. Halafu vipi hoja ya Waziri ikijibiwa kwa hoja, badala ya viroja?

Respect.

FMEs!

mzee FMes; unadhani sijui kuandika clearly kuwa "ninapendekeza sheria zetu zibadilishwe kusudi iwe halali kuvuta bangi ili kuwapa vijana nafasi ya kugombeai"? sishindwi kuandika hivyo, kwa hiyo sikuwa ninahalalisha kuvuta bangi kama unavyotaka kupotosha post yangu. Uvutaji bangi ni kosa la jinai, lakini ni jukumu la mahakama kutoa hukumu hiyo. Huwezi kusema kwa vile unadhani mtu fulani anavuta bangi basi hafai kuwa kiongozi wakati mahakama haijamwona na hatia hiyo ya kuvuta bangi. Nimetoa mifano ya watu waliowahi kuvuta bangi na wakakiri kufanya lakini hawakuonekana na hatia mbele ya mahakama hivyo waliweza kuwa marais wa merakani.

Mwambie ndugu yako mzee Wassira aache kugeneralize kuwa vijana wote ni wavuta bangi na kijana akishavuta bangu tu basi hafai kuwa kiongozi; huo ni udhalilishaji mbaya sana kwa vijana wetu ambao tunadai kuwa ndio wajenzi wa taifa hili. Kama yeye ana ushahidi kuwa vijana wote ni wavuta bangi basi awafikishe mahakamini ili wahukumiwe kisheria badala ya kutoa matusi kwa vijana wote nchini bila msingi wowote.
 
Hivi Wasira ambaye havuti bangi amelifanyia nini taifa katika kipindi chote hicho akiwa kama mbunge?
 
Wassira amesahau alikotoka!!!!!!!!!!!!!

Alimaliza darasa la nane hapo Kyarano Middle School...kaingia Chama cha Ushirika, Ushashi...zao la pamba!

Kapigania u-Bunge kwa mgongo wa washirika wa Ushashi.

Kapita na hapo baadaye kufanywa Waziri mdogo wa Kilimo...shauri ya kuwa mkwe wa Chifu Wanzagi Nyerere.

Kisha kapewa kazi huko u-balozi wetu washington, DC.

Kaanza kusomea digrii ya kwanza na hatimaye kamaliza MA!

Ana bahati sana.

Lakini kaanza kama KIJANA SAAAAAAAAAAANA!

Sasa anawakataa vijana nao wasigombee...basi acheni bangi vijana!
,
 
Wasira anaogopa kurudi kijiweni Jojis alipokuwa anaomba supu ya kongoro ,amshukuru kijana wake JK kwa kumukumbuka,sasa kumbe waimba taarabu wana vision ndio maana waliimba Mtu mzima ovyooo kumbe walijua akina Tyson watakuwepo
 
....hana lolote anaweza fanya zaidi ya kukaa bungeni…..

Haya ndiyo maneno. Kabla ya kuwa mkwe wa Chifu Wanzagi Nyerere inasemekana alikuwa anauza samaki mtaa kwa mtaa (yaani kama wale wauza mchicha wa mitaani). Kwa msoto huu inawezekana sana hata bangi alivuta
 
kazi kweli kweli, yani mtu anaona Ubunge kama ni halali kwake tu. Wala alikuwa hana haja ya kutoa hii kauli, manake Ubunge ni haki ya yoyote anayetimiza masharti ya kuwa Mbunge. Kivuli cha kina Mzindakaya na Kimiti!!!
 
Mengine mnamuoneya kabisa; Wassira hajawahi kuishiwa pesa kiasi cha kuomba supu au kutembeza samaki. Alikuwa anasafirisha samaki kwenda nchi za nje na ingawa malipo yalikuwa siyo makubwa lakini alikuwa hana shida ya pesa kiasi hicho. Tatizo kubwa alilokuwa nalo ni kule kukosa madaraka baada ya kuwa nayo kwa miaka 26 mfululizo. Kitendo cha kujikuta na raia wa kwaida asiyekuwa na hata punje ya daraka kilikuwa kinamsumbua sana kisaikolojia.

Pamoja na yote hayo, Wassira ana historia ndefu sana iliyojaa bahati na mafanikio makubwa sana kisiasa. Kwanza siyo kweli kuwa alipewa madaraka kwa sababu ya kuoa binti wa Nyerere. Nitaeleza histroia yake kadri ninavyomfahamu.

Stephen Masato Wasira alisoma Nyambitilwa kule Ushahi na kumalizia darasa la nane pale shule ya kati ya Kisangwa. Baada ya hapo alijishughulisha na shughuli za TYL ambayo ilikuwa inasimamiwa na Kiboko Nyerere (mdogo wa Nyerere); hivyo alianza connection angali mdogo sana. Akiwa kwenye TYL akafanikiwa kupata kazi ya serikali kama Bwana Maendeleo huko Ukerewe. Wakati akiwa Ukerewe, alijza form ya kugombea Ubunge wa Mwibara baada ya mbunge wa wakati huo Chiliko kuwa mkuu wa Wilaya huko Shinyanga. Katika kipindi cha uchambuzi wa wawagombea, Wassira akapata nafasi nyingine mjini Musoma kuwa katibu mtendaji wa TANU wa wilaya ya South Mara. Katika kinyang'anyiro kile cha ubunge wa Mwibara, Wassira alipambana na mtu anaitwa Muyenjwa, ambaye alikuwa Division Executive Secretary wa tarafa fulani hivi. Ushindi wa Wassira katika uchaguzi ule wa 1970 ulitokana na tabia ya dharau na ukatili wa Muyenjwa katika madaraka aliyokuwa nayo wakati ule; kwa hiyo watu wakamwadhibu Muyenjwa kwa kumnyima kura na kumpa mpinzani wake (yaani Wassira) ambaye alikuwa hafahamiki - hiyo ilikuwa bahati ya kwanza ya Wassira.

Akiwa mbunge, Wassira alichaguliwa kuwa waziri mdogo wa Kilimo mwaka wa 1972 kufuatia reshuffle iliyofanywa na Nyerere baada ya mauaji ya sheikh Karume; alikaa katika madaraka hayo kwa miaka kama miwili au mitatu hivi ambapo mwaka 1974 akateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kuchukua nafasi iliyoachwa na Ackland Mhina alipokwenda kuwa balozi wetu huko nje. Akiwa Mkuu wa mkoa ndipo alipooa mtoto wa chief Wanzagi Nyerere; kwa hiyo siyo kweli kuwa alipewa madaraka kwa kuwa alikuwa ameoa kwa Nyerere, No, alioa kule wakati akiwa na madaraka. Inawezekana ndoa ile ilimuimarisha katika nafasi ile ya ukuu wa mkoa kwa sababu alikaa pale Musoma hadi mwaka 1983, yaani karibu miaka 9 hivi. Kuna madudu kadhaa aliyofanya pale Musoma ambayo sitayataja kwa vile sina ushahidi nayo ila mwanzoni mwa mwaka 1983 watu wa Musoma walimwambia Mwalimu waziwazi pale kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mukendo kuwa, atakapoondoka kurudi Dar es Salaam baada ya mapumziko yake ya krismas ni lazima aondoke na mtu wake (yaani Wassira)- wao walikuwa hawamtaki tena. Kwa vile Nyerere alikuwa hataki kuwaudhi zaidi ndugu zake wa Musoma (unawajua jinsi walivyo wakali), kweli akafanya hivyo; mwishoni mwa mwaka 1983 hiyo hiyo Wassira akaondolewa pale Musoma na kuwekwa Mambo ya Nje alikoishia ubalozini Washington, DC. Nashindwa kutambua kama hapo alikuwa na bahati au alikuwa amejiunganisha vizuri kisasa, lakini hakusota.

Katika uchaguzi wa mwaka 1985, Wassira aligombea jimbo la Bunda ambalo wakati huo lilikuwa linashikiliwa na Mugeta. Kwa bahati mbaya kama ilivyokuwa kwa Muyenjwa, Mugeta naye alikuwa na ishu zake kiasi kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Bunda aliyekuwa akijulikana kama Munubi Salamu, alianza kupiga kampeini kuzuia Mugeta asichagulie katika uchaguzi ufuatao, na badala yake mpinzani wake ndiye apewe kura hata kam wakati huo mpinzani halisi alikuwa hajajulikana. Baada ya jina la Wasira kuibuka, mzee Salamu akageuka ili kupiga kampeini FOR Mugeta, lakini hakuweza kuponyesha damage aliyokuwa keshafanya. Hivyo Wassira akachaguliwa kama njia ya kumwadhibu Mugeta - Hiyo ilikuwa ni bahati nyingine.

Baada ya ushindi huo Wasira akawa waziri mdogo wa serikali za mitaa na ushirika na baadaye akawa waziri kamili nadhani wa kilimo. Katika nafasi zake za uwaziri alizifanya kwa ufanishi wa kuridhisha sana, na hivyo kwa karibu miaka karibu 10 yote iliyofuata hadi 1995, Wassira alikuwa madarakani.

Hata hivyo wakati wa uchaguzi wa 1995 alijikuta akishindana na waryoba kupitia CCM na hivyo akaenguliwa kulingana na uzito aliokuwa nao waryoba kichama. Kwa mabavu yake, waryoba akahamia NCCR mageuzi ambako alishinda kiti cha Bunda dhidi ya Waryoba. Kulikuwa na ukweli kuwa Wassira alitumia njia chafu sana katika uchagzui ule ili kumshinda waryoba, hivyo mahakama kuu ikatengua ubunge wake na kumzuia asigombee position yoyote kwa miaka mitano. Kipindi hicho ndicho Wassira alipokaa benchi na pia hakuweza kushiriki uchaguzi wa mwaka 2000 kutokana na amri hiyo ya mahakama. Mwaka 2005 akagombea tena Bunda na kushinda hadi kuwa waziri, kazi aliyo nayo hadi sasa. Ushindi huo wa 2005 nadhani aliupata kutokana na jina lake kuwa kubwa na vile vile mbinu zake za kisiasa kuwa zimekomaa; ushindi huo haukuwa wa bahati tena.

Hata hivyo, kutokana na historia yake, ni wazi kuwa Wassira hana profession yoyote nje ya siasa. Kuna wanasiasa ambao walikuwa na profession zao kabla ya kuingia kwenye siasa lakini Wasira siyo mmoja wao - yeye ni career politician.
 
mzee FMes; unadhani sijui kuandika clearly kuwa "ninapendekeza sheria zetu zibadilishwe kusudi iwe halali kuvuta bangi ili kuwapa vijana nafasi ya kugombeai"? sishindwi kuandika hivyo, kwa hiyo sikuwa ninahalalisha kuvuta bangi kama unavyotaka kupotosha post yangu. Uvutaji bangi ni kosa la jinai, lakini ni jukumu la mahakama kutoa hukumu hiyo. Huwezi kusema kwa vile unadhani mtu fulani anavuta bangi basi hafai kuwa kiongozi wakati mahakama haijamwona na hatia hiyo ya kuvuta bangi. Nimetoa mifano ya watu waliowahi kuvuta bangi na wakakiri kufanya lakini hawakuonekana na hatia mbele ya mahakama hivyo waliweza kuwa marais wa merakani.

Mwambie ndugu yako mzee Wassira aache kugeneralize kuwa vijana wote ni wavuta bangi na kijana akishavuta bangu tu basi hafai kuwa kiongozi; huo ni udhalilishaji mbaya sana kwa vijana wetu ambao tunadai kuwa ndio wajenzi wa taifa hili. Kama yeye ana ushahidi kuwa vijana wote ni wavuta bangi basi awafikishe mahakamini ili wahukumiwe kisheria badala ya kutoa matusi kwa vijana wote nchini bila msingi wowote.

- Unajua something is worng somewhere na hizi hoja, maana kila kiongozi ni ndugu yangu, habari iliyoletwa haiko kamili lakini kama ilivyo,

- Wassira amesema anawajua wanaotaka kumtoa kwenye ubunge ni vijana wavuta bangi, sasa labda angeulizwa facts, sasa kwa vile hakuulizwa basi ni valid argument kwa maoni yangu, sasa hoja yake ijibiwe kwa hoja thats all!

Respect.

FMEs!
 
Wasira served as Deputy Minister of Agriculture in the first phase Government under President J.K.Nyerere and also served as the Deputy Minister for Local Government and later as the Minister of Agriculture and Livestock Development under second phase President A.H. Mwinyi

He was appointed as Minister of Water on January 4, 2006, when Jakaya Kikwete , who had been elected President, named his new cabinet. He was then moved to the position of Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives on October 15, 2006, and on February 12, 2008 he was named Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government.

Education
BA in Economics, American University, in Washington, DC, USA.
BA in Political Science, American University, in Washington, DC, USA.
MA in Economics, American University, in Washington, DC, USA.
Masters in Public Administration, American University, in Washington, DC, USA.

Positions held
Member of Parliament - Mwibara Constituency 1970 - 1975
Deputy Minister of Agriculture 1972 - 1975
Regional Commissioner Mara Region 1975 - 1982
Minister Counselor at the Embassy of Tanzania, Washington, DC, USA - 1982 - 1985
Member of Parliament - Bunda Constituency 1985 - 1990
Deputy Minister for Local Government 1987 - 1989
Minister of Agriculture and Livestock Development 1989 - 1990
Regional Commissioner Coastal Region 1990 - 1991
Member of Parliament - Bunda Constituency 1995 - 1996
Member of Parliament - Bunda Constituency 2005 - Present
Minister for Water - January 2006 - October 2006
Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives - October 2006 - February 2008
Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government - February 2008 - May 2009
Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives May 2008 - Present
 
Swali kubwa sana ambalo huwa najiuliza ilikuwaje Mzee wasira aliyekwenda DC bila degree akapata degree nne katika kippindi cha miaka mitatu. Naomba mwenye historia hii atueleze. maana hapa sijawahi kupata jibu.
 
Tatizo wanajua kwamba kura yetu haina nguvu ndio maana wanapata jeuri yakuongea chochote wanachojisikia. Wanajeuri mno kwani wengi wao wanaona kazi ya ubunge ni ya milele.
 
Sijui ni kwa lengo gani hasa, lakini kuna upotoshaji kwenye habari hii. Alichosema Wasira ni kuwa ujana kisiwe kigezo pekee cha kuwafanya wagombea wengine wenye umri mkubwa kama Wasira kukosa sifa ya kugombea. Ndipo akasema kuwa unaweza kujikuta unamuachia kijana mvuta bangi kwa kuwa tu ni kijana.

Hii imenikumbusha maneno ya mwalimu pale Kilimanjaro Hotel 1995 aliposema kuwa mtu anapofilisika kisiasa (Kukosa hoja) hutafuta kujihalarisha kibaguzi ama kwa kabila yake, au umri wake nk.

Wakubwa tuliowapa madaraka wamaetufanyia madudu mengi sana kama EPA, Richmond nk. Badala ya kuwahoji kuhusu haya, tunakubali kudanganywa nao nasi kama yale makondoo ya Animal farm tunaishia kuimba ujana, ujana..., Are we cursed?
 
Ni kweli kabisa miaka 5 hv nyuma hali yake ilikuwa mbaya sana acha atapetape na amshukuru sana JK maana sasa ingekuwa hali mbaya sana sana .....naona uwezo wake ulishafikia kikomo wana bunda wafanye la msingi sasa....kama tangu 1970 hajafanya la maana hata yeye hajafanya lake la kumfanya apumzike akitoka pale hatuna zaidi wana Bunda acheni utindio wa ubongo kwenye kufikiri!!
 
Wassiraalifikiria kuwa kutoka Amerika Nyerere angemtunukia wadhifa mkubwa. Cheza na kambarage! Kambarage alimtupa nje.

Kupigania ukubwa: Wassira akawa so frustrated na kujitoa CCM. yeye na mwana-Diplomsia mwenzake Wedi Mwasakafyuka waliunda chama chao kipya; wakaishiwa mafuta upesi upesi!

Wassira akabaini ni vyema arudi kwao,CCM!
 
duh kumbe madongo ya jumla jumla yanauma!

Inawezekana kwamba kauli ya Mzee Wassira imepotoshwa kama mdau alivosema hapo juu. Hata hivyo jinsi mtiririko wa hii thread inavyokwenda inaonekana jinsi vijana wasivyopendezwa na madogo ya jumla jumla kuhusu ujana.

Hivi hatuoni madongo ya jumla jumla wanayopigwa wazee hapa JF? Mara wazee kazi kulala, mara "vijizee" mara nyingine "lizee" mradi ubaguzi wa kiumri. Wazee tuwaheshimu na tuwapinge kwa hoja na wala si vioja.

Ama kweli mkuki kwa nguruwe...
 
Wasira served as Deputy Minister of Agriculture in the first phase Government under President J.K.Nyerere and also served as the Deputy Minister for Local Government and later as the Minister of Agriculture and Livestock Development under second phase President A.H. Mwinyi
He was appointed as Minister of Water on January 4, 2006, when Jakaya Kikwete , who had been elected President, named his new cabinet. He was then moved to the position of Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives on October 15, 2006, and on February 12, 2008 he was named Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government.
hivi kwa sasa hivi wasirra ni waziri katika ofisi ya prime minister na utawala wa mikoa na serikali za mitaa? hizi data/kumbukumbu zinatoka wapi? ndio maana wassira anaongelea wavuta bange miongoni mwetu.

Education
  • BA in Economics, American University, in Washington, DC, USA.
  • BA in Political Science, American University, in Washington, DC, USA.
  • MA in Economics, American University, in Washington, DC, USA.
  • Masters in Public Administration, American University, in Washington, DC, USA.
Positions held
Member of Parliament - Mwibara Constituency 1970 - 1975
Deputy Minister of Agriculture 1972 - 1975
Regional Commissioner Mara Region 1975 - 1982
Minister Counselor at the Embassy of Tanzania, Washington, DC, USA - 1982 - 1985
Member of Parliament - Bunda Constituency 1985 - 1990
Deputy Minister for Local Government 1987 - 1989
Minister of Agriculture and Livestock Development 1989 - 1990
Regional Commissioner Coastal Region 1990 - 1991
Member of Parliament - Bunda Constituency 1995 - 1996
Member of Parliament - Bunda Constituency 2005 - Present
Minister for Water - January 2006 - October 2006
Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives - October 2006 - February 2008
Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government - February 2008 - May 2009
Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives May 2008 - Present

source:http://en.wikipedia.org/wiki/stephen_wasira

Back
Top Bottom