Wasira: Siachii ubunge kwa vijana ni wavuta bangi..!!!


Term limits (say two terms) za ubunge zitaondoa aina ya Mibunge kama hii........
 
hivi kwa sasa hivi wasirra ni waziri katika ofisi ya prime minister na utawala wa mikoa na serikali za mitaa? hizi data/kumbukumbu zinatoka wapi? ndio maana wassira anaongelea wavuta bange miongoni mwetu.
Hayo yameandikwa kwenye mtandao angalia tanzania politician
 
Huyu Wasira amshukuru sana marehemu Mzee Kawawa kwa kumpigia debe kurudishwa CCM ama sivyo mpaka leo angekuwa anauza samaki pale Namanga!! Anaposema vijana hawafai kuwa viongozi kwavile wanapuliza ganja ana maana hawa wakina Ngeleja, Hussein Mwinyi na Masha wamepewa ujiko na muungwana japo wanalipuuliza ganja? Wasira anazeeka vibaya na yote hiyo sababu ya njaa; pale kilimo anamuangusha Jakaya, jamaa hafanyi lolote la maana ila ni kuiba tu!!
 
Dawa ya watu kama wassira ni kutafuta vijana wenye uwezo na kuwasimika Bunda, tupige kambi kule hadi ang'oke... tuhimize vijana wote wachukue kadi za CCM, wote washiriki kwenye mchujo wa mgombea CCM halafu tupige kura; tukishamaliza tunaacha fair competition kati ya huyo kijana na wapinzani wote

Wassira is living in the past!!! Let us show him the power of our young generation
 
Kichuguu,
Hivi yule mama mkwe wa Wassira, mwalimu wangu Radegonda, alikuwa mke wa Chief Wanzagi kweli? Nitawauliza akina Lucy na Flora. Ukweli ni kuwa hata mpige kelele gani Wassira haondoki kwenye siasa angalau kwa sasa. Ni mmoja wa mawaziri wanaojua kuzitumia taasisi zilizo chini ya wizara anayopewa kuiongoza.
 
Wasira anfikiri vijana peke yao ndio wavuta bangi hata wazee nao huvuta bangi kwani yeye halijui hilo. Jamaa hapa karopoka. Anafikiri yeye ndo anamua? Ni wapiga kura ndo huamua nani awe Mbunge na sio yeye. Aende zake amefulia.
 
Kuna kipindi alidata hadi akafanya biashara ya sato kuleta mjini. wacheni atafute hela za uzeeni -
 
- Wassira siku zote ni mwanasiasa mjanja sana, Warioba aliposhika kiti chake cha ubunge alimpeleka majuu asirudi kumsumbua, ni mmoja wa wanasiasa wa kwanza sana kujiunga na Mtandao kwa siri, ndio maana sasa anachuma matunda yake!

- Na ni almost awe PM kama sio wazee wa nchi kuingilia kati! yupo mpaka Mtandao uishe nguvu! na akiona unaisha kama kawa ataruka viunzi na kuwahi wapya wenye nguvu zaidi! maana huko kwao ana ujanja flani unaowashinda wengi!

Respect.


FMEs!
 
Wakubwa, mbona mmeisahau mizee mingine nayo ina kauli hizo hizo? Mbona hata Makweta kasema hivyo, na Malechela? Wote manyang`au tu hawa, 2010 tuwapige chini!
 
Warioba hakumpeleka majuu Wassira.
 
Huyu naye sasa anachemsha. Anajeuri gani ya kusema kuwa aachi ubunge? Kwa mtazamo wangu, wapiga kura wake ndo wenye uwezo wa wakusema kuwa aachie au asiachie.

Ningekuwa mimi ni kijana kwenye jimbo lake la uchaguzi nisingempigia kura kabisa, kwani amemaanisha vijana wote ni wavuta bangi, wakati wao ni sehemu kubwa ya kura zilizomweka madarakani.

Hawa vijani wa jimbo lake wambane ili aoneshe wavutabangi anaowataja na akishindwa wafungulie mashtaka.
 
Wassira naye ni one of those 'bushed' polititians ambao wameishiwa sera vichwani wanaishia kutoa maneno ya kibaguzi yenye kukera. We are not at 'war' here between the old and young. Hata statement yake itafsiriwe vipi amefanya kosa la kudhalilisha vijana kwamba hawafai kuachiwa uongozi na kwa sababu ya bangi.

What is being suggested/asked is that at least wazee ambao wamekuwa wabunge tangu ujana wao wawaachie na wengine hususan vijana wa sasa nao washike nafasi hizo. Is that unreasonable and too much to ask to warrant insulting the youth?
 
Hii ndiyo jeuri ya viongozi wetu. Wanafikiri ni haki yao peke yao kuwa wabunge. Ndiyo maana wakisikia mwingine anagombea wanaanza kujiliza oh anatumiwa na mafisadi, oh wanataka kuchukua jimbo langu....what is this?
 
Wassira naye ni mvuta bangi ,na tena huenda naye anamiliki shamba la Bangi ndio maana akajua kuwa vijana wanavuta kwani wanaenda kununua kwake.
 
Mwenye historia yake kifamilia, I mean mke, watoto, atumuvuzishie....
 
mwenye historia yake kifamilia, I mean mke,watoto, atumuvuzishie....

Mimi ninajua familia yake vizuri lakini sidhani kama ina maana yoyote kuzungumza mambo ya familia yake kwenye forum kama hii kwa vile wao hawajihusishi na siasa. Ni lazima tuheshimu privacy yao kwa vile hawajataka kujiweka hadharani. Kuna viongozi ambao mambo ya familia yao ni haki ya kila mtanzania kwa vile familia nzima zimejikita kwenye siasa, lakini familia ya Wasira haiko hivyo; kwa hilo ni lazima tuwaheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…