ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Nyundo ya Mahakama Je inaweza kuwa ndio mwisho wa huo ujanja ujanja wa kutembeza bakuli la tonetone? 🤣🤣
Pia soma Breaking News: - Pre GE2025 - Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA
Ni Kutiki tuu hiyo Oktoba
===
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna mtu au kikundi cha kuzuia uchaguzi huku akiwataka wananchi kujiandaa kutiki na kutobabaishwa na kaulimbiu ya ‘no reform no election’ ya CHADEMA kwa kuwa inakwenda kufikia mwisho.
Pia amewasisitiza Watanzania na wanachama wa chama hicho kujiandaa kwenda ‘kutiki’ kwa kumpigia kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan na mwenza Dk. Emmenuel Nchimbi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Wasira ameyasema hayo leo wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma wakati akizungumza na wanachama wa CCM, viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya kijamii.
“Usibabaishwe na maneno hakuna mtu wa kuzuia uchaguzi, utakuwepo na ninyi mabalozi toweni watu wetu waende wakapige kura muda ukifika, waende ‘wakatiki’ na tiki yenyewe ni rahisi maana unaona CCM na alama ya jembe na nyundo.
“…Utamuona mgombea wetu Dk. Samia na Dk. Nchimbi halafu mbele ya hao watu unaweka tiki. Kwa hiyo nilitaka niwaeleze haya mambo muyajue vizuri ili msije kubabaishwa," amesema Wasira.
Source: Nipashe