PreGE2025 Wasira: Wananchi jiandaeni Kutiki, No reforms Inaelekea Mwisho

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mkuu, Ni kwamba unaandika ukiwa hujui aina ya majibu yaliyopo au basi tu inabidi uandike sababu ushajikatia tamaa? Ukijibiwa hakuna mpasuko kwani NRNE hawafiki hata laki tano, wapo mitandaoni una namna ya kupinga?

Swali la kujiuliza, inashindikana vipi kwa walio wengi kutengeneza attention nchi ikatulia kuwasikiliza?

Huu mtego ukiweza kuutegua unachosema kitapaswa kuwa na matokeo otherwise ni porojo zisizo na mtokeo bila kujali ni kweli au la.
 
Unaposema wanaoamini kwenye No Reform, No Election hawafiki laki 5 una uthibitisho gani? Unafahamu idadi kamili ya wanachadema nchi nzima? Ajenda ya No Reform, No Election ni ya CDM lakini imeungwa mkono na wasio CDM sasa tafuta kwanza idadi ya wanachama wa CDM nchi nzima halafu ongeza na wale washabiki tu ambao wapo hata ccm kisha fanya tathmini ya jumla. Wewe unadhani kwanini ccm haitaki tume huru kama kweli ina watu kuliko CDM.
 
Huyu mzee kaanza kula keki ya Taifa kabla haijaokwa akaila jikoni mezani hadi jalalani ilikotupwa leo unadhani atakupa story gani? Mirija yake yake yote iko huko atakuambia nini kuhusu reform asichotambua No reform No Election iliwhatoka kwa CDM imekua agenda ya yeyote anaelitakia mema Taifa hili hizo hadaa watakuja kuumbuka vibaya wananchi kwa sasa sio wale wa miaka ile ya TV za chogo wangesoma alama za nyakati
 

Attachments

  • 20250610_184844.jpg
    115.9 KB · Views: 22
Bado hujasema
 
Huyu mzee asibabaishe watu ,anatakiwa kaa chini na kujitafakari ni miaka mingapi imebaki mbele yake , hii dhuluma anayopalilia hata matunda yake wenda asiyaone Mungu yupo kazini
 
Sawa mzee Wasira nimejiandaa kutiki kwa CHAUMMA
 
Unaposema wanaoamini kwenye No Reform, No Election hawafiki laki 5 una uthibitisho gani?
Wewe una uthibitisho gani kwamba wanafika? Unauliza swali lile lile ambalo umekuwa ukichapwa nalo wakati wa matokeo ya uchaguzi.
Unafahamu idadi kamili ya wanachadema nchi nzima?
Unarudi tena pale pale, kama idadi inatosha ni nini kisichofanyika kinachosababisha kuangukia pua?
Ajenda ya No Reform, No Election ni ya CDM lakini imeungwa mkono na wasio CDM sasa tafuta kwanza idadi ya wanachama wa CDM nchi nzima halafu ongeza na wale washabiki tu ambao wapo hata ccm kisha fanya tathmini ya jumla.
Unang'ang'ana na idadi, unaitumiaje? Umekuwa ukiitumiaje? Kwanini hii idadi haina msaada kwenye matokeo?
Wewe unadhani kwanini ccm haitaki tume huru kama kweli ina watu kuliko CDM.
Idadi unayoisema haina uwezo wa kulazimisha tume huru ya uchaguzi na ikasikilizwa? Hiyo ni idadi kibogoyo, idadi hewa au idadi unafiki?
 
CCM hawawezi kutawala hii nchii kwa miaka 10 ijayo labda wabadilike waache wizi na wawekeze kwenye uchumi vijana wapate ajira.
 

View: https://www.instagram.com/p/DKz7yl9NBhm/?igsh=aTcyZnU1ZjRuNnMw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…