Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira amevitaka vyama vya upinzani kuacha kuwa na visingizio katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi badala yake wakubali kushiriki uchaguzi ili washindane.
Akiwa Tukuyu, mkoani Mbeya Machi 20 Wasira amesema
"tunataka waje ulingoni waache visingizio waje maana timu inayoona itafungwa mara nyingi ndiyo inayokimbia uwanjani"
Soma pia:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wasira ametumia mfano wa timu inayoogopa kuingia uwanjani kuwa itafungwa akimaanisha wanaoogopa kushiriki uchaguzi wanahofia kushindwa kwenye chaguzi hizo.
"Ukiona timu imeogopa kuja uwanjani ina mashaka kuwa itafungwa kwa hiyo tunaviambia vyama njooni acha kuweka mpira kwapani"
Aidha kwa siku za karibuni timu iliyokataa kwenda uwanjani kushiriki mchezo ni Simba Sc ambayo ilikataa kwenda kucheza na Young Africans Sc kitendo ambacho baadhi walitafsiri kama uoga wa Simba huku wao wakisema walifanyiwa vurugu kunyimwa kufanya mazoezi ya mwisho.