Pre GE2025 Wasira: Watanzania hawana sababu ya kuichagua CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewajibu vikali wanaodai kuwa hakuna kilichofanyika tangu Tanzania ipate uhuru, akisema kuwa kauli hizo zinatokana na kutojua historia ya maendeleo ya nchi.

Akizungumza katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, Wasira amesema kuwa maendeleo yaliyofikiwa ni makubwa na yanaonekana wazi, huku akisisitiza kuwa CCM imeendelea kutekeleza maono ya ukombozi wa kisiasa na kiuchumi kutoka kwa vyama vilivyoasisi uhuru wa nchi- TANU na ASP.

"Wapo wanaosema miaka 60 hakijafanyika chochote, lakini ni kwa sababu hawajui wanachokisema. Mimi niliijua Tarime kabla ya uhuru, na leo hii Tarime ni tofauti kabisa. Watu wa Tarime wa sasa wanajua kusoma na kuandika, wana huduma bora za afya, na miundombinu imeimarika," amesema Wasira.

Ameendelea kueleza kuwa serikali ya CCM imeleta mabadiliko makubwa nchini, hasa ndani ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwamo ujenzi wa madarasa mapya na vituo vya afya vyenye vifaa vya kisasa.

Wasira pia ameikosoa CHADEMA, akidai kuwa chama hicho hakina mshikamano wala ajenda zenye tija kwa wananchi.

"Juzi wamefanya mkutano Dar es Salaam, wamegawana fito. Mmoja kaenda na ya kwake, mwingine kaenda na ya kwake. Hicho ni chama kweli? Halafu wanakuja kuwaambia watu wa Tarime wawapigie kura kwa sababu gani?" amehoji Wasira.

Amewataka wananchi wa Tarime kuendelea kuiamini CCM kama chama pekee kinachotekeleza maendeleo ya kweli kwa Watanzania.
 
Attachments

  • 1edaac7a3e34dc7dbc36bb899a6e6430_1738702701936.mp4
    5.4 MB
Amezungumza ofisini na wananchi au waandishi wa habari?
Aliozungumza nao wameruhusiwa kumwuliza maswali?!
 
Kama wapo wanaosema kuwa hakuna kilichofanyika wanaikosea sana CCM inamaana hata wizi wa kura hawauoni?.
 
Noma sana,kama ccm bado wanawatumia wazee wa miaka 80 kwenye nafasi nyeti kama ya mzee Wasira,basi huko kwenye chama hakuna watu
 
Back
Top Bottom