Wasiwasi wangu juu ya mradi wa Maabara ya akili bandia iliyozinduliwa UDOM

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
394
Reaction score
720
Chuo kikuu cha Dodoma( kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wamezindua Mradi wa Maabara ya akili Bandia (Artificial Intelligence) kwa Maendeleo ya Afrika

Mradi huu ni kama wa matumizi ya roboti ambao utalenga kutengeneza mashine ambazo zitakuwa zinafanya kazi za kutumia akili kama binadamu.

Mradi umezinduliwa na naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe. Mohammed Khamis katika ukumbi wa mikutano Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu

Hongera sana udom kwa jambo hilo kubwa kwenye teknologia ya sasa

Lakini wasiwasi wangu hadi nikaandika huu uzi

Je, haya mambo ya robotics hayatamaliza kabisa Ajira hata hizi chache zilizopo
Maan kama kitu kitaweza kufanya kazi kama binadamu maanake sasa kazi nyingi zitafanywa na robot
Au hii imekaaje wadau.
 
Tanzania na robotics/AI bado sana....wala usiwe na wasiwasi juu ya ajira...
 
... artificial intelligence tafsiri yake ni akili bandia?
Hata mimi nimejiuliza hilo swali, kwa uelewa wangu akili bandia ni fake intelligence au nakosea mkuu
 
... vichekesho kweli kweli! Halafu ndio tunataka lugha adhimu itumike hadi elimu ya juu nyanja zote - sayansi, sheria, utabibu, uchumi, etc. kwa kigezo eti mbona hata Japan, China, Germany, Russia, et. al. wanatumia lugha zao!
 
Jina bandia linapoteza maana halisi ya artificial intelligence.
 
TUMEWEKEZA VYA KUTOSHA? WATAALAM WAPO WA KUTOSHA AU NDIO BORA LIENDE
 
... vichekesho kweli kweli! Halafu ndio tunataka lugha adhimu itumike hadi elimu ya juu nyanja zote - sayansi, sheria, utabibu, uchumi, etc. kwa kigezo eti mbona hata Japan, China, Germany, Russia, et. al. wanatumia lugha zao!
Au tiziite akili za kisasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo kikuu cha Dodoma( kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wamezindua Mradi wa Maabara ya akili Bandia (Artificial Intelligence) kwa Maendeleo ya Afrika

Mradi huu ni kama wa matumizi ya roboti ambao utalenga kutengeneza mashine ambazo zitakuwa zinafanya kazi za kutumia akili kama binadamu.

Mradi umezinduliwa na naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe. Mohammed Khamis katika ukumbi wa mikutano Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu

Hongera sana udom kwa jambo hilo kubwa kwenye teknologia ya sasa

Lakini wasiwasi wangu hadi nikaandika huu uzi

Je, haya mambo ya robotics hayatamaliza kabisa Ajira hata hizi chache zilizopo
Maan kama kitu kitaweza kufanya kazi kama binadamu maanake sasa kazi nyingi zitafanywa na robot
Au hii imekaaje wadau.
If you live in the past the future will never find you
 
Back
Top Bottom