onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,356
- 1,309
Tumeibiwa kuku, ng'ombe, mbuzi na kukwapuliwa simu hatujawahi kusikia wala kuona nguvu za jeshi la akiba. Kimsingi hawa sijui walikuwa wanaitwa Sungusungu au Mgambo lakini kwa nature ya kazi yao ilikuwa kupambana na uhalifu mdogo mdogo vijijini. Kwenye kampeni ziazoendelea jana wameibuka Shinyanga.
Swali la kujiuliza hivi polisi na jeshi la wanachi wamezidiwa hadi kuletwa jeshi la akiba. Tuko vitani na nani hadi sasa kuletwa jeshi lingine? Je, hii si mbinu ya kutengeneza makundi ya kijeshi ili kudhibiti upinzani na kuwatia watu hofu?
Hivi CCM kwanini wanataka kutuingiza katika sintofahamu? Mbona vyama vingine wao wamejikita kunadi sera na wao wanahaha kutafuta majeshi? Hofu ya CCM ni nini hasa?
Wito wangu ule msemo wa kufanya kampeni za kistaarabu kusiwe ni kupaka upepo matope bali uwe kwa vitendo. CCM wakinukisha hAta watoto wao nao watanukishiwa tu.
Janjajanja ndio maana Lissu na Membe wanakubalika.