Uchaguzi 2020 Wasiwasi wangu ni hili 'Jeshi la akiba' muda huu wa kampeni

Uchaguzi 2020 Wasiwasi wangu ni hili 'Jeshi la akiba' muda huu wa kampeni

Kwanini uogope jeshi Kama huna nia mbaya?
Lazima kuogopa, kwani yawezekana ndio wale wasiojulikana? Toka lini CCM wakawa na nia nzuri? Kama CCM ingekuwa na nia nzuri tusingekuwa hapa kwenye uchumi wa kati, tungekuwa uchumi wa kwanza.
 
Mhutu anavyopenda kumwaga damu lazima amewaandaa kumwaga damu sio bure
IMG_20200901_130103.jpg
IMG_20200901_130114.jpg
 
Mgombea wenu hajui kama kuna sheria ya People's militia, hata hivyo kusaidia ulinzi wa mkutano wako ni kukandamiza wanyonge? Wakiwepo Polisi mkutanoni anawatukana ati wanatumika, wamemletea vijana wa jeshi la akiba wasio na silaha wawasaidie nao anawafukuza
Kwanini zamani hawakuletwa?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Vyombo hivi vipo miaka yote tena kisheria vikisimamiwa na jeshi la polisi maarufu kama Sungusungu au kwa Dar vinajulikana kama Ulinzi Shirikishi. Jeshi la Polisi kwa uchache wa askari haliwezi kuwa sehemu zote, hawa ni msaada mkubwa. Mfano ni wakati huu wa kampeni, Priority ya Polisi ni kulinda misafara na mikutano ya Magufuli ambaye mbali na ugombea yeye bado ni Rais
Hamna kitu hapo, huu ni uhuni mwengine wa ccm ktk sura hii.
 
Hawa ni vijana wa ccm waliokuwa wamewekwa kambini mwaka jana na mwaka huu...karibia kila wilaya Tanzania imetoa vijana wake kujiunga na mafunzo ya ukakamavu na medani za vita
Hilo ni kundi kubwa na hatari kabisa na halipaswi kupuuzwa hata siku moja...wamefanyiwa brainwash ya kutosha sana kuhusu upinzani

Kulikuwa na ratiba na bajeti maalum kwa ajili ya hayo makundi na walipelekwa kwenye makambi ya siri kwa wiki tatu tatu ...mwezu na nk
Bajeti ilijumuisha
Malipo kwa ajili ya wakufunzi
Chakula
Malazi
Mavazi
Vinywaji
Posho nknk
Vyanzo vya mapato vilikuwa toka kwa wafanyabiashara na wenye viwanda vikubwa na vya kati...hawa walipelekewa barua za kuomba michango ya hali na mali pamoja na bajeti....chochote kilipokelewa na michango iliratibiwa na makada wa ccm toka makao...
Hao vijana ni kundi kubwa na wameiva hasa...kuna hao wenye uniform lakini nyuma yao wana backup ya wasio na uniform na wamefunzwa kuwasiliana kwa lugha ishara na wanatambuana kwa ishara na kila mmoja ana code number yake....

USINIULIZE NIMEJUAJE[emoji848][emoji2827][emoji848][emoji2827][emoji848][emoji2827][emoji848][emoji2827]
 
Hawakuletwa sababu polisi hawakuwapo wa kutosha. Rais nae yupo Shinyanga ulitegemea nani awe na ulinzi wa Polisi wa kutosha kati yake na Rais?
Kumbe polisi hawakutosha kwanini serkal isiajiri vijana wengi waliokosa ajira hasa toka JKT. Kwanini iamue kutumia kikundi cha watu? Hela si zipo si makusanyo ya kodi ya me double sana kwnn ajira hamna?pesa znaenda wapi?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la akiba? ni katiba ipi inayoruhusu jeshi la akiba au ni sheria ipi inayohalalisha jeshi la akiba?

Katiba inampa Amiri Jeshi Mkuu mamlaka kuunda vikosi vya majeshi kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na usalama wa raia.
 
Katiba inampa Amiri Jeshi Mkuu mamlaka kuunda vikosi vya majeshi kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na usalama wa raia.


Tutajie hicho kifungu nasi tukisome mkuu
 
Sheria tunazijua vizuri hii hapa inatamka kuanzisha jeshi la akiba wakati wa vita sio wakati wa uchaguzi , Jiwe anajiaandaa kumwaga damu maana yeye bila kumwaga damu hajisikii
Screenshot_20200903-205934.png
 
Tumeibiwa kuku, ng'ombe, mbuzi na kukwapuliwa simu hatujawahi kusikia wala kuona nguvu za jeshi la akiba. Kimsingi hawa sijui walikuwa wanaitwa Sungusungu au Mgambo lakini kwa nature ya kazi yao ilikuwa kupambana na uhalifu mdogo mdogo vijijini. Kwenye kampeni ziazoendelea jana wameibuka Shinyanga.

Swali la kujiuliza hivi polisi na jeshi la wanachi wamezidiwa hadi kuletwa jeshi la akiba. Tuko vitani na nani hadi sasa kuletwa jeshi lingine? Je, hii si mbinu ya kutengeneza makundi ya kijeshi ili kudhibiti upinzani na kuwatia watu hofu?

Hivi CCM kwanini wanataka kutuingiza katika sintofahamu? Mbona vyama vingine wao wamejikita kunadi sera na wao wanahaha kutafuta majeshi? Hofu ya CCM ni nini hasa?

Wito wangu ule msemo wa kufanya kampeni za kistaarabu kusiwe ni kupaka upepo matope bali uwe kwa vitendo. CCM wakinukisha hAta watoto wao nao watanukishiwa tu.

Janjajanja ndio maana Lissu na Membe wanakubalika.
Hahahahhaha dah Rejea Ukubaliji Wa Dr Slaa Halafu utaambie maana ya kukubalika
 
Hili Jeshi ni rasmi?Mbona hatuwaoni kwenye mikutano ya CCM popote tangia kampeni zianze rasmi?Hawa ndiyo wasiojulikana?
CCM Mpya mnahofia kushindwa uchaguzi huu,ila Majeshi ya Akiba yameandaliwa kuwadhibiti wapinzani/Chadema.
Mkuu hiki Ni kikundi kilichoanzishwa na mbunge wa chadema Rachel Mashishanga kwa ajili ya kulinda usalama kwenye shughuli za chadema, Salome Makamba alivyoingia alikitelekeza, ndio kikaanza kufanyakazi huru, kimsingi Ni Mali ya chadema,
 
Back
Top Bottom