Uchaguzi 2020 Wasiwasi wangu ni hili 'Jeshi la akiba' muda huu wa kampeni

Hoja sio majina, kila eneo wanatohoa majina yao, Dar ni Ulinzi shirikishi. Hoja ni mgombea Urais asiyejua mifumo ya ulinzi wa nchi uliopo kisheria😬
Jeshi la M23 ya magu. Hapo hakuna jeshi la akiba. Hapo ukifanya upembuzi utakuta kumechanganyika na magwiji wenye mafunzo makali kabjsa ya kijeshi. Anatupiga changa la macho. Tumemshtukia. Intelijensia ya chadema ni kali sana.
 
Soma Katiba. Sura ya uanzishwaji wa majeshi ya ulinzi na usalama

Mkuu kama mayai yanapanda soma mchango wa Chief Kabikula #38 hapo utatoa tongotongo au kama nawe unayo nyingine weka hapa tuijadili
 
Leteni tu vurugu tuwanyooshe
 
Sungusungu/ulinzi shirikishi "mnajioganizi"wenyewe kwenye mtaa wenu au kijiji na gharama mnazibeba wenyewe.Mgambo wameenda wapi?
 
Unajitah
Mkuu hiki Ni kikundi kilichoanzishwa na mbunge wa chadema Rachel Mashishanga kwa ajili ya kulinda usalama kwenye shughuli za chadema, Salome Makamba alivyoingia alikitelekeza, ndio kikaanza kufanyakazi huru, kimsingi Ni Mali ya chadema,
Unajitahidi kuwatetea Intarahamwe?Kama ni kikosi kilichoundwa na huyo MwanaCHADEMA uliyemtaja,ni sawa yeye kufanya hivyo?Sheria za nchi hii zinafanyaje kazi?Kila makosa yanayofanywa na watawala yakihojiwa mnayahusisha na wapinzani.Je,ndio wanaounda serikali inayohitajika kutupa ukweli wa yale tunayoulizia?
Hivyo vikosi vya Jeshi la Akiba ni haramu hata kama vimeundwa/kutumika na nani hapa nchini.Hawapo kisheria na tunapoulizia uwepo wao tupo sahihi na tunastahili kufahamishwa.Nimewaona wengine kwenye Canter nyeupe yenye Plate No.ya PT,yawezekana ni shopped photo?
 
Sungusungu/ulinzi shirikishi "mnajioganizi"wenyewe kwenye mtaa wenu au kijiji na gharama mnazibeba wenyewe.Mgambo wameenda wapi?
Hoja ni wapo kwa sheria? Rais ajaye alikuwa Ubelgiji hajui hilo. Waalipwa na nani sio hoja!! Kwani hao mgambo huwa wanalipwa na nani? Au vijana wanaojitolea wakirudi nyumbani wanalipwa na nani? Ndiyo maana ya Jeshi la Akiba.
 
Red brigade iliasisiwa na mbowe na ndio hao wanamlinda yeye, mbona hahoji wanaomlinda Ni kea Sheria ipi?
 
Jeshi la M23 ya magu. Hapo hakuna jeshi la akiba. Hapo ukifanya upembuzi utakuta kumechanganyika na magwiji wenye mafunzo makali kabjsa ya kijeshi. Anatupiga changa la macho. Tumemshtukia. Intelijensia ya chadema ni kali sana.

Ukiwaza hivyo, hata Jeshi la JKT, JKU na Mgambo livunjwe maana wanafunzwa vikali ikiwemo matumizi ya silaha za Kivita na tunao mtaani. Kila nchi ina namna yake ya kudhibiti uhalifu. Kwa sera yetu ya ulinzi, Tanzania kila raia ni mlinzi wa nchi ndiyo maana kuna AMANI. Waliozaliwa 90's hawajui hili.
 
Hatari inainyemelea nchi yetu huku tunazuiwa hata kuhoji hali hiyo.Akijitokeza mtu wa kulizia hilo ataitwa CDM/Mpinzani.
 
Hakuna cha jeshi la akiba wala nini hao ni wahalifu wa "green guards" wapo kazini.

Hamna kitu hapo, huu ni uhuni mwengine wa ccm ktk sura hii.

Hao vijana wanatumika kwa namna ambayo wao hawajielewi... Ni sawa na wale wahuni waliotumwa kutupa mawe ktk mkutano wa TL...

Ni hatari kuwa na vikundi au majeshi yasiyo rasmi Kama hayo..
 
Kwa hiyo chadema wanaogopa mgambo kuliko jeshi la police,
Pia wao hawaruhusiwi kusikiliza mkutano?
 
Hao vijana wanatumika kwa namna ambayo wao hawajielewi... Ni sawa na wale wahuni waliotumwa kutupa mawe ktk mkutano wa TL...

Ni hatari kuwa na vikundi au majeshi yasiyo rasmi Kama hayo..
Naam, CCM inawatumia kiutapeli. Zoezi la kukusanya hao vijana lilianza zaidi ya mwezi mmoja ulio pita. Wajumbe wa serekali za mitaa ndo wanaotumika kuwatafuta. Wanawaambia wazazi / walezi kuwa wanapelekwa jeshini, na vigezo ni umri wa miaka 18 na lazima wapewe kadi za ccm.
Huko Magu jamaangu kanambia zoezi hilo limehitimishwa juzi. Inshort ni mwendelezo wa utapeli wa ccm.
 
Unazungumzia jeshi gani la wananchi inaonekana hata hajui mipaka ya majeshi yetu.
 
Hata mkitangaza kuongeza mishahara wakati wowote kuanzia sasa pasipo Bunge kupitisha,tutawapiga chini tu.
Maoni ya mdau wa jf
 
Mkuu kama mayai yanapanda soma mchango wa Chief Kabikula #38 hapo utatoa tongotongo au kama nawe unayo nyingine weka hapa tuijadili

Kimsingi, post #38 mchangiaji amenukuu National Defense Act ambayo inanazungumzia mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu katika kuanzisha majeshi wakati wa Vita.

Katiba katika Sura ya Unzishaji wa Majeshi, inazungumzia kwa ujumla mamlaka ya aliyopewa Amiri Jeshi Mkuu kuanzisha na kuunda majeshi.

Kwa hiyo, ukizingatia tafsiri ya National Defense Act kwamba Amiri Jeshi Mkuu ana mamlaka ya kuunda Jeshi wakati wa Vita pekee unakuwa unakiuka Katiba ya nchi na unapotosha.

Katiba haijasema kwamba Amiri Jeshi Mkuu ana mamlaka ya kuunda majeshi wakati wa Vita pekee, bali inasema Amiri Jeshi Mkuu ana mamlaka ya kuunda vikosi vya majeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…