Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Hello Wadau
Nimekuwa niki-bet mara kadhaa na pia kupitia mikeka ya Tipsters mbalimbali. Lakini wasiwasi wangu mkubwa ni juu ya hili wimbi kubwa la Tipsters mitandaoni wanaozidi kuongezeka wengine wakiwa hao wachambuzi wa soka.
Nilichogundua hawa Tipsters wengi wanaingia mikataba na kampuni za kubet, wewe unaweza kudhani wanatoa mkeka bure kumbe wenzako wanapata commission kutoka hayo makampuni kadri wanavyoleta watu kupitia referral links au betting codes.
Vilevile kuwa makini wakati unachukua mikeka yao, maana mingine imetengenezwa hili uingizwe chaka. Unakuta mkeka una timu 10, ila mtego upo kwenye timu mmoja hiliyopewa option ambayo hata namna gani hiyo option haiwezi kushinda. Mnachukua mikeka yao bila kukagua options, unaweka badae unaliwa alafu Tipsters anakupoza kuwa ni timu moja tu iliyochana, kumbe ulikuwa mpango wa kupuruswa. Alafu badae anaweka mkeka mdogo wa odd 2 wa kweli kukupoza.
Hivyo kuweni makini na Tipsters ambao sio waaminifu.
Tipster asiye mwaminifu anaweza kufanya mambo yafuatayo:
- Kupokea kamisheni za rufaa kutoka kwa kampuni za ubashiri, huku akiwahamasisha watu kuweka dau nyingi kupita kiasi.
- Kuuza utabiri wa uongo kwa makusudi kwa watu wanaolipia huduma zake za betting tips, huku akiifaidisha kampuni ya kubeti na baadae anapewa commission.
- Kutangaza matokeo fulani ya mechi huku yeye mwenyewe akiweka dau kwenye matokeo tofauti kwa siri.
- Kutengeneza au kughushi tiketi za ushindi ili kuwavutia wateja wapya na kuwafanya waamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kutabiri matokeo ya mechi.
NB: Bet kistaarabu, kagua options za mikeka za Tipsters kuangalia high chances, usimwamini Tipster mazima. Usichukue tu betting code na kui-paste kwako moja kwa moja. Wengi wao wanaingia mikataba na haya makampuni ya kubet.
Taja Tipster mmoja unayemjua ambaye ni kanjunju na mwingine mwenye afadhali