Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 6,585
- 10,363
Happy Easter to everyone,
Nimeguswa ku share haya machache kuhusu hili kundi kubwa la watu (Wasomi) ambalo ndo linaongoza kulalamika huku mitandaoni kuwa maisha magumu na wengine wakienda mbali zaidi kuwa serikali yetu haiwajali.
Nimefuatilia kwa ukaribu wasomi wengi, kitu kinachowakwamisha ni wao wenyewe kujiona wao ni tofauti na watu wengine kwenye jamii na wanastahili kupewa heshima kubwa.
Huu mtazamo wenu wasomi ndo unawafanya mnapishana na fursa nyingi kwakua lazima tukubali hakuna serikali duniani iliyoweza kuwaajiri watu wake wote , hivyo basi ukiwa kama msomi na umekosa ajira cha kwanza kabisa kubali kujishusha kuendana na mazingira halisi ya mtaani.
Elimu uliyo nayo isikufanye uzubae tuu jichanganye na watu wa mtaani walioanza ujasiriamali hata kama wanafanya kwa kiwango cha chini, kupitia kujichanganya kwako kutakuongezea maarifa ambayo huna.
Elimu uliyo nayo isikufanye kujiona kuwa wewe ni mtu wa hadhi ya juu, huku huna source yoyote ya kukuingizia kipato. Kama huna means yoyote ya kuingiza kipato basi ujue kuna vingi sana huvijui unapaswa ujifunze.
Elimu uliyo nayo itakusaidia tuu endapo utakubali kubadilika kutokana na mazingira lakini pia kukubali uhalisia wa mambo coz huku mtaani mambo ni tofauti sana na vile wasomi wanavyochukulia pindi wakiwa vyuoni.
Elimu ulionayo ukiongeza na maarifa kidogo tuu utakayoyapata pindi ukijichanganya na watu mtaani itakua na faida sana, kuliko kusubiri ajira.
Elimu uliyo nayo bila kuwa na pesa tambua fika hakuna atakayekupa heshima kama wengi wenu mlivo na mawazo hayo ya kijinga.
Kushinda mitandaoni na kulalamika kuwa ajira ngumu tuu bila kuchukua hatua zozote ni ujinga ambapo ni wa kuacha mara moja.
Tunawategemea sana kuja kuleta ukombozi mtaani kutokana na elimu mlioipata, ila hii hali ya kulaumu tuu serikali inatupa sana mashaka kuwa kuna uwezekano tuna wasomi ambao hawajaelimika.