Udhaifu mkubwa wa sera ya Chama Cha Mapinduzi.
Yaani kule ulaya Kila mwezi wanatunza data za Unemployment rates na kupush vijana kwa kuwapa back-up inayoweza wasaidia eidha wajiendeleze au waishi wakisubiri ajira zingine.
Ila kwetu hakuna data za Unemployment rates za Kila mwezi, hatujui watu unemployed wako wangapi watengeneze sera za kuwaalika foreign investors wajenge viwanda vya kuwaajiri vijana, Leo hii kijana anatoka na 4.5 GPA tena honourable anakaa mtaani na ideas zake murua alizopambania miaka yote zikipotea bila matumizi yoyote alafu Serikali inashinda inanunua ma-V8 na kutengeneza miradi ambayo ndani yake kuna upigaji wa ajabu yalioanikwa na CAG, si Bora hizo pesa wawape vijana ambao hawaajajiliwa ila wanareport taarifa zao pale National Bureau of Statistics huku wakiendelea kusaka ajira zingine.
Hii kitu Cha "Kujiajiri isiwe ndo hoja ambayo Serikali inaitumia kupoteza vijana kufikia ndoto zao".
Imagine mtu anatoka chuo, anadaiwa almost 10 million na HESLB, Hana ajira, kaamua kujiajiri, bado hajakutana na wale wa TRA pasua kichwa, Kuna wengine wanatoka chuo hawana kitu, walikuwa wanalisha familia zao masikini, je mtawapa mtaji?
Mikopo hii ya Samia imejaa nepotism na corruption, kama wewe huna mtu wa CCM kama connection, hupati utapoteza muda sana.
SERIKALI IKAE CHINI NA KUANZA KUKUSANYA DATA WAONE UNEMPLOYED WANGAPI WAWEZE KULITATUA TATIZO, EIDHA WAPUNGUZE MAKODI YA AJABU WAWARUHUSU FOREIGN INVESTORS WAJE.