Wasomi hawa tulio nao vyuo vikuu, ni sawa?

Matukio yote hayo huwa
yanaandaliwa na jopo la wanazuoni, mimi nazungumzia msukumo binafsi
walionao wasomi.

Ukiona wanafunzi wengi wanahudhuria kigoda cha Nyerere ujue wanafata
kifungua kinywa cha bure kama kipindi kile cha mwaka juzi.

Mkuu mi mbona nliwahi kuiwinda ile capachino nlishndwa nlikuta washakunywa....nikarud zangu Mabibo kulala
 
Mkuu mi mbona nliwahi kuiwinda ile capachino nlishndwa nlikuta washakunywa....nikarud zangu Mabibo kulala

Kuna moja tuliigonge Yombo 5, na msosi wa mchana ukapigwa Nkrumah kwa nje, mbona mugambo waliruka na kukanyagana?
 
Mkuu hilo nalo neno matokeo yake kila kitu huendeshwa kisanii maghorofa yana anguka kwa ujenz wa kisanii yaan!Tuombe..
 

Nadhani tunapojaribu kuchangia hoja hii iliyo mbele yetu ni vema tukaelewa kwamba tunapokuwa (sisi au vyombo vya habari) tunaongelea habari za wenzetu walioaga dunia tunasukumwa sana na mchango wake kwa taifa na wala sio kiwango chake cha elimu aliyonayo, au mahali na taasisi anakofanya kazi. Nawaheshimu sana wasomi wetu ila si kweli kwamba wao ndio pekee wenye kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu. Wapo watu wengi waliotoa mchango mkubwa kwa taifa letu na hawakuwa wasomi (Marehemu Kanumba ni mmoja wao kwani alitumia maarifa yake kama msanii kuajiri watu na kulitangaza taifa letu na pengine serikali yetu ingekuwa makini ingefaidika [pengine ilifaidika] kutokana na kodi ya mauzo ya rekodi zake nje na ndani ya nchi). Tusipumbazwe na degree au uprofesa wa hawa waitwao wasomi. Kwanza ukijaribu kuchambua kwa umakini watu wanaochangia kwa sehemu kubwa kuirudisha nyuma nchi yetu kimaendeleo ni hawahawa tunaowaita wasomi. Wakati mwingine nitaeleza kinagaubaga ni kwa namna gani wasomi hawa (sio wote, ila walio wengi) wanachangia sana ktk kudidimiza maendeleo ya nchi yetu.

Tukikaa tukidhani maendeleo yanaletwa na wasomi tu, tunajidanganya. Kwanza wasomi wetu wengi wana-frustrations kibao. Tusidanganye katika hili... Wapo wasanii wengi waliotoa mchango unaotukuka kwa taifa letu kuliko wasomi hawa ambao kwanza wakipata nafasi serikalini ndo wanakuwa wezi na mafisadi wa kutupwa kabisa. Angalia maprofesa na madaktari wetu wengi walioamua kuingia kwenye siasa na uchambue mchango gani wameutoa kwenye sekta zao kama sio kuleta migogoro na wakati mwingine ubabaishaji tu. Angalia sekta ya Elimu, angalia Ardhi na Nyumba/Makazi, Maji n.k. Hao wasomi waliosimamia sekta hizo wameleta tija gani tangu waingie????

Kwa msingi huo, mimi nawapongeza sana TV/Redio Mlimani kwa uzalendo waliouonesha kumpa heshima mtanzania mwenzetu aliyetutoka ila akaacha mengi ya kumkumbuka kuliko profesa anayekufa kwa jina tu "profesa". Haisaidii!
 
Then mwsho wa cku wanajiita wao ni bora kwa kipi hasa?
Wamebakiza jina2 medula zao hamna k2
 
Usiwe biased! Kanumba anamchango mkubwa japo kama si mfuatiliaji ni ngumu kuuona. Kwa kazi zake wengi wameajirika, wametoka, wamejulikana kimataifa na kuifanya ardhi yetu ikajulikana. Anamengi ya kusifiwa. Ni mfano wa kuigwa kwa kujiajiri.

eti nini? anamchango mkubwa! upi? kwa akili yako inamaana bila kanumba ardhi yetu haitajulikana?!! au unataka kuniambia hata wakoloni waliijua iliyokuwa TANGANYIKA kupitia Kanumba?. hapa hakuna llolote zaidi kuharibu watoto wetu hadi wanapokuwa madarasani shule na kwenye mitihani wanachokumbuka ni maneno na mistari ya wasanii mabwenyenye! hujani convince bado.
 
SAWA!! Lakini Kanumba anatija gani mpaka watu vyuoni watenge rasilimali muda kuadhimisha kifo chake?!!
 
Inaonekana akitokea mdau awaambie waache shule awalipe milioni kila mwezi wataacha hawa,kwa kuwa wana ndoto za kupata maisha bora kwa shotkat... Kuna usomi tena hapo?

umeonaeee!!!! wasomi uchwara!
 

A great thinker
 

Na ndio maana sijakurupuka kutaja wasomi tu, maaan hata Kikwete nae ana Ph.D (regardless ameipataje), nimetaja wasomi ambao walau wana mcahango wa maendeleo chanya kwa taifa.

Maadhimisho ya siku ya Kanumba yalikuwa powered na Clouds FM, wala sio utambuzi wa mchango wake, ndiposa hawa wasomi kama wanavyounga tela kwa kila kitu wakaunga tela na hili...
 
Baba yako Mama yako, mkeo mtoto wako wamekufa hata tarehe za kufa kwao hukumbuki lakini unamkumbuka kanumba,tuacha ulimbubeni
 
Nadhani weledi wa mtu si hoja sana inapokuja kwenye coverage kwenye media zetu, ila nadhani umaarufu ni muhimu zaidi. Proresaz ni maarufu kwa wasomi wenzao, whereas wasanii ni maarufu kwa watu wote akiwemo hata mtoto wangu amabaye hata kindergatten hajaanza
 
Then mwsho wa cku wanajiita wao ni bora kwa kipi hasa?
Wamebakiza jina2 medula zao hamna k2

Hakika nakuambia, kama Mlimani a.k.a Chuo cha Taifa hali ni mbaya namna hii, basi huko kwenye vyuo vya kata hali ni mbaya mara dufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…