Nadhani tunapojaribu kuchangia hoja hii iliyo mbele yetu ni vema tukaelewa kwamba tunapokuwa (sisi au vyombo vya habari) tunaongelea habari za wenzetu walioaga dunia tunasukumwa sana na mchango wake kwa taifa na wala sio kiwango chake cha elimu aliyonayo, au mahali na taasisi anakofanya kazi. Nawaheshimu sana wasomi wetu ila si kweli kwamba wao ndio pekee wenye kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu. Wapo watu wengi waliotoa mchango mkubwa kwa taifa letu na hawakuwa wasomi (Marehemu Kanumba ni mmoja wao kwani alitumia maarifa yake kama msanii kuajiri watu na kulitangaza taifa letu na pengine serikali yetu ingekuwa makini ingefaidika [pengine ilifaidika] kutokana na kodi ya mauzo ya rekodi zake nje na ndani ya nchi). Tusipumbazwe na degree au uprofesa wa hawa waitwao wasomi. Kwanza ukijaribu kuchambua kwa umakini watu wanaochangia kwa sehemu kubwa kuirudisha nyuma nchi yetu kimaendeleo ni hawahawa tunaowaita wasomi. Wakati mwingine nitaeleza kinagaubaga ni kwa namna gani wasomi hawa (sio wote, ila walio wengi) wanachangia sana ktk kudidimiza maendeleo ya nchi yetu.
Tukikaa tukidhani maendeleo yanaletwa na wasomi tu, tunajidanganya. Kwanza wasomi wetu wengi wana-frustrations kibao. Tusidanganye katika hili... Wapo wasanii wengi waliotoa mchango unaotukuka kwa taifa letu kuliko wasomi hawa ambao kwanza wakipata nafasi serikalini ndo wanakuwa wezi na mafisadi wa kutupwa kabisa. Angalia maprofesa na madaktari wetu wengi walioamua kuingia kwenye siasa na uchambue mchango gani wameutoa kwenye sekta zao kama sio kuleta migogoro na wakati mwingine ubabaishaji tu. Angalia sekta ya Elimu, angalia Ardhi na Nyumba/Makazi, Maji n.k. Hao wasomi waliosimamia sekta hizo wameleta tija gani tangu waingie????
Kwa msingi huo, mimi nawapongeza sana TV/Redio Mlimani kwa uzalendo waliouonesha kumpa heshima mtanzania mwenzetu aliyetutoka ila akaacha mengi ya kumkumbuka kuliko profesa anayekufa kwa jina tu "profesa". Haisaidii!