Wasomi mnatukera, kuoa muoe nyie pesa tuchange sisi!

Wasomi mnatukera, kuoa muoe nyie pesa tuchange sisi!

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Kuna mambo yanakera na kuchukiza, hebu fikiri yaani mtu unaungwa kwenye group la Whatsapp bila taarifa, ukifuatilia purpose la group unaambiwa group la bwana nani eti kwa lengo la kuchangisha michango kwa ajili ya harusi x. Yaani inakera na kuchukiza, nyie wasomi wa kibongo hii nchi sasa si ya Kijamaa ni ya Kibepari.

Unatuomba michango sisi for what reason wakati kuoa unaoa wewe na mbususu unakula wewe? Chefuuu! Badilikeni aisee, mnakera na kuchukiza. Binafsi mimi harusi yangu marufuku mtu yoyote yule kuchangia aisee.
 
Huuu upuuzi inabidi ifike mahali uishe kabisa!! Mtu anaoa atafute namna ya kufanya anayotaka kufanya kwa budget zake mwenyewe sio kutegemea watu!!

Unaweza funga ndoa kirahisi tu mkapata cheti bila shamrashamra za kusumbua watu!!
 
Michango noma sana uunajikita kwenye magroup kama mayano hivi halafu wanaweka na minimum kabisa eti 70k , sasa tuma elfu 10 uone gubu lake kana kwamba kimaidha tunalingana

Mi policy ni moja tu, ukiniadd kwenye group la mchango wa 50k naitafuta hiyo hela kisha 25k natuma kwenye mchango hiyo 25k namtumia Bibi yangu kijijini, haiwezekani nichangie watu wacheze kwaito siku moja wakati Bibi yangu hiyo anaserebuka nayo wiki nzima na zaidi
 
Back
Top Bottom