Wasomi mpo?

Wasomi mpo?

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
461
Reaction score
392
Msomi mmoja mwenye PHD pamoja na kijana mmoja ambaye hakubahatika kwenda shule walisafiri pamoja kwenda kutembelea mbuga moja maarufu yenye maua na ndege wa kuvutia.

usiku ulipofika wakaweka hema lao zuri na la kisasa na wakalala usingizi mzito kabisa.

Msaa machache baadae, Yule kijana asiye msomi akamwamsha yule msomi na kumwambia:"angalia angani na niambie nini unaona ?"

Jamaa mwenye PHD akajibu:"Naona mamilioni ya nyota na mbalamwezi" Yule kijana asiye msomi tena akauliza "Unajifunza nini ukiona hivyo?"

Yule msomi akatafakari kwa dakika kadhaa kisha akajibu:

"kiunajimu inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi sana katika hii dunia kwetu wanadamu.

Kwa upande wa muda inaonyesha ni usiku wa manane na pia kwa upande wa imani inadhihirisha kuwa Mungu ni muweza wa vyote na sisi kwake ni viumbe wadogo sana na tusio na mamlaka.

Kwa upande wa wanahewa ni kwamba kesho itakuwa siku nzuri sana. Kwa upande wako wewe inakuambia nini?"

Yule jamaa asiye msomi akakaa kimya kwa muda na kisha akasema: "Kiuhalisia …… Inaniambia mimi kuwa …."Hema letu limeibiwa!!
 
hhahahahah .. duniani huku PhD na level nyingine za Masomo ni mbwembwe tuu .
akili ni mtu binafsi... hahahaha
 
hahaha inachekesha lakin mi naona msomi alikua sawa kwa upande wake coz huyo kijana aliuliza unaona nin angan ilo swal lilikua general sana
 
Kali sana hii, sam taim wasomi huwa wanakwama padoogo sana mpaka mtu unapata mashaka na kiwango chake cha elimu!
 
Back
Top Bottom