Wasomi, Nifafanulieni Hii Hesabu iliyotumiwa Hapa.


Ni sawa mkuu, lakini ulichokifanya kimahesabu hakina tofauti na nilichokifanya, ni suala la sehemu na asilimia tuu, ndo inakufanya uweze kupata majibu ya swali hilo, mwingine anaweza kugawa vipande sita kwa kila mkate, au kama mimi nilivyoenda moja kwa moja kuigawa mikate 8 kwa watu watatu na majibu yangu mengi kuwa kwenye sehemu. Ni mambo ya kukumbuka tuu unachokifanya.
 


Ha ha ha ha!! hizi hesabu bwana!! yaani wewe umeamua kuanzia kwenye majibu kabisa?? hiyo 7000 ya kuanzia umeitoa wapi?? kwani ungeweza kuulizwa kuwa ungekuwa ni wewe hiyo 8000 aliyotoa wa tatu ungeigawa vipi?? sasa wewe kwa sababu kakupa kila kitu unatafuta kianzio kwenye majibu?? hata kama ingekuwa ni ku prove mimi hapo sikupi marks maana hakuna kazi uliyoifanya.
 
Prof Gamba majibu yako hayajatulia X-PASTER mjibu yako ni sahihi japo step #1 hukuonesha ni jinsi gani umepata hivyo vipande 24, swali ni zuri na linasolvika kiuraisi kwa probabilistic maths without forcing some steps

Wapi panapotia shaka kwenye maelezo yangu mkuu?? maana nimeamua kuanzia mwanzo na kutoa maelezo ya nilichokuwa nakifanya.
 


Respect mkuu, umesomeka vizuri sana.
 

"mmoja alinunua mikate mitano (5) na mwinginee mitatu (3).. Aliye nunua mikate mitano (5) achukuwe shilingi efu saba (7,000) na aliyenunua mikate mitatu (3) achukuwe shilingi elfu moja (1,000). Je hakimu alitumia fomula gani katika kugawa haki?"

mkuu umeelewa swali linataka nini? swali ni kuprove hapo bold na mimi nimetumia probabilistic approach, Mzawa Halisi ametumia njia za finance (if not mistaken) na kupata majibu yaleyale.... nilianza kulifanya kabla ya kuona majibu kama sheria za maths zinavyosema.. hili swali hata mtoto wa form 2 analifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…