Wasomi, Nifafanulieni Hii Hesabu iliyotumiwa Hapa.

Wasomi, Nifafanulieni Hii Hesabu iliyotumiwa Hapa.

<>Majibu<>


  1. Mikate: 8, ukigawa kila mkate vipande vitatu sawa 1/3 jumla vipande vitakuwa 24.
  2. Wamekula sawa kwa sawa, ina maana kila mmoja kala vipande 8. 1=8 x 3 = 24
  3. Yule wa mikate mitano (5) atatoa vipande 15 = (3 x 5 = 15) kwenye mikate yake, na amekulaa vipande 8 na kubakia vipande 7 = (15 - 8 = 7)
  4. Yule wa mikate mitano (3) atatoa vipande 9 = (3 x 3 = 9) kwenye mikate yake, na amekulaa vipande 8 na kubakia kipande 1 = (9 - 8 = 1)
  5. 7 ya kwanza jumlisha na 1 unapata vipande nane (8) alivyokula yule wa tatu.
  6. Kimahesabu, yule wa tatu kala Kipande kimoja (1) cha yule aliyetoa mikate 3 na kala vipande saba (7) kwa yule aliyetoa mikate 5... Kimalipo uwiano (ratio) ni 7:1

Ni sawa mkuu, lakini ulichokifanya kimahesabu hakina tofauti na nilichokifanya, ni suala la sehemu na asilimia tuu, ndo inakufanya uweze kupata majibu ya swali hilo, mwingine anaweza kugawa vipande sita kwa kila mkate, au kama mimi nilivyoenda moja kwa moja kuigawa mikate 8 kwa watu watatu na majibu yangu mengi kuwa kwenye sehemu. Ni mambo ya kukumbuka tuu unachokifanya.
 
kwa kutumia probabilistic approach
assume wa 3 amelipa exact amount (8000/=) kwa alichokula. hakimu amegawa hela (8000/=) based on contribution of everyone to jamaa wa 3
wa mikate 5 amecontribute 7000/8000 = 7/8 kumlisha wa 3
wa mikate 3 amecontribute 1000/8000 = 1/8 kumlisha wa 3
7/8+1/8 = 8/8 = 1

ukitaka kujua kila mmoja alitoa vipande vingapi (X) kwa jamaa wa 3 fanya hivi

7/8 * 8 = 7 (kwa jamaa wa kwanza)
1/8 * 8 = 1 (kwa jamaa wa pili)
--> kwahiyo jumla alikula vipande = 7+1 = 8 hence ni sawa kabisa na kusema kila mmoja alikula vipande 8!
--> jumla vililiwa vipande 8 * 3 = 24

note: swali halijasema kama mikate yote ililiwa na halijasema kila mkate ulikatwa vipande vingapi

kudadadeki ng'ombe hazeeki maini


Ha ha ha ha!! hizi hesabu bwana!! yaani wewe umeamua kuanzia kwenye majibu kabisa?? hiyo 7000 ya kuanzia umeitoa wapi?? kwani ungeweza kuulizwa kuwa ungekuwa ni wewe hiyo 8000 aliyotoa wa tatu ungeigawa vipi?? sasa wewe kwa sababu kakupa kila kitu unatafuta kianzio kwenye majibu?? hata kama ingekuwa ni ku prove mimi hapo sikupi marks maana hakuna kazi uliyoifanya.
 
Prof Gamba majibu yako hayajatulia X-PASTER mjibu yako ni sahihi japo step #1 hukuonesha ni jinsi gani umepata hivyo vipande 24, swali ni zuri na linasolvika kiuraisi kwa probabilistic maths without forcing some steps

Wapi panapotia shaka kwenye maelezo yangu mkuu?? maana nimeamua kuanzia mwanzo na kutoa maelezo ya nilichokuwa nakifanya.
 
Njia fupi:

watu watatu waligawana sawasawa, hivyo kila mmoja alikula 1/3
Ambaye hakununua alilipa shilling 8,000 ambayo ni sawa na 1/3 ya gharama ya mikate yote.
Hivyo thamani ya mikate yote ni 8,000 * watu 3 = 24,000
Kwa vile mikate ilikuwa nane, basi mkate mmoja ni shilling 3,000
Yule aliyenunua mikate mitatu alitoa shillingi 9,000 na wa mikate mitano alitoa 15,000.
Ili kila mmoja kuchangia sawa, aliyetoa 9,000 atarudishiwa 1,000 na yule wa 15,000 atarudishiwa elfu saba na kufanya wote kuwa wametoa 8,000.


Respect mkuu, umesomeka vizuri sana.
 
Ha ha ha ha!! hizi hesabu bwana!! yaani wewe umeamua kuanzia kwenye majibu kabisa?? hiyo 7000 ya kuanzia umeitoa wapi?? kwani ungeweza kuulizwa kuwa ungekuwa ni wewe hiyo 8000 aliyotoa wa tatu ungeigawa vipi?? sasa wewe kwa sababu kakupa kila kitu unatafuta kianzio kwenye majibu?? hata kama ingekuwa ni ku prove mimi hapo sikupi marks maana hakuna kazi uliyoifanya.

"mmoja alinunua mikate mitano (5) na mwinginee mitatu (3).. Aliye nunua mikate mitano (5) achukuwe shilingi efu saba (7,000) na aliyenunua mikate mitatu (3) achukuwe shilingi elfu moja (1,000). Je hakimu alitumia fomula gani katika kugawa haki?"

mkuu umeelewa swali linataka nini? swali ni kuprove hapo bold na mimi nimetumia probabilistic approach, Mzawa Halisi ametumia njia za finance (if not mistaken) na kupata majibu yaleyale.... nilianza kulifanya kabla ya kuona majibu kama sheria za maths zinavyosema.. hili swali hata mtoto wa form 2 analifanya
 
Back
Top Bottom