Kwanza Nikujuze ndugu mleta uzi ,Kinachotafutwa Ni Kinga na sio dawa...
Sasa nije kwenye swali kwamba Wataalam watanzania wako wapi wakati wenzao wa Nchi nyingine wakihangaiaka kutafuta suluhu ya Corona???
Wakati Fulani Swali Hujibiwa kwa Swali/Maswali ..
Hivyo basi, Tujiulize..
Je Tanzania imewahi kufanya Uwekezaji wowote serious kwenye Tafiti? Hasa katika kutenga Fungu la fedha kuwezesha watafiti??Kuna maazimio kadhaa yamewahi kuwekwa Kama vile kutenga 1% ya pato la Taifa iende kwenye Tafiti, Je limewahi kutekelezwa au iliishia kwenye makaratasi??
Je Tuna Maabara za viwango vya juu Kama hizo zinapofanywa Tafiti za Corona katika First World Countries?? Hapa Usisahau kuwa Maabara inayotumika kuthibitisha maambukizi ya Corona Ni moja tu Hadi Sasa Nchi nzima!
Katika Vipaumbele vya sekta ya Afya Tanzania na Nchi nyingine za Dunia ya tatu Kuna uwezekano wowote wa kutenga mabilioni ya Fedha kwenye kutengeneza "Facilities" kwaajili ya Tafiti Kama za Nchi ya Dunia ya Kwanza Huku wakati huohuo nchini mwao kukiwa na changamoto nyingine zenye ulazima zaidi Kama vifo vya kinama wajawazito, utapiamlo, upungufu wa vituo vya afya n.k ambazo zinademand fedha pia??????
Kwanini Wataalam wa Kiafrika hufanya makubwa Sana katika Nchi za Ulaya na America lakini katika Nchi zao hawafanyi lolote????
NB;
Sisi Kama Nchi tupambane na matatizo saizi yetu,kutokana na uwezo wa Facilities zetu na Nguvu zetu za kiuchumi..Hakuna namna tuanze kujenga First class Labs zitakazocost Billions wakati vitu vya msingi tu kama Utapiamlo na Udumavu kwetu Bado ni changamoto .It doesn't make sense .
"Rome wasn't built in a Day" hivyo hakuna muujiza utakaotokea ghafla bin vuu tuanze kushindana na Nchi Kama Marekani na Israeli kwenye Tafiti za kisayansi...
Wataalam wa Kitanzania na Afrika wana uwezo mkubwa kufanya hata zaidi ya hayo yanayofanywa na wenzetu..Tatizo ni mazingira..
Ili mbegu iote inahitaji vitu Kama maji/unyevu na mwanga kuota..
Ukiitupa mbegu Jangwani au Gizani Usitegemee au Usije kuiuliza mbegu baadae " Kwanini wewe hujaota wakati wenzio waliopo kandokando ya mto wanatoa matunda" ....
Sent using
Jamii Forums mobile app