Wasomi wa afya na Wakemia Tanzania, mbona kimya kuhusu ugunduzi wenu wa dawa ya Coronavirus?

Wasomi wa afya na Wakemia Tanzania, mbona kimya kuhusu ugunduzi wenu wa dawa ya Coronavirus?

Kama unatumia fake ID umri humu ndani unapimwa kwa michango yako. Ww kama ni mtu mzima basi ni wale hovyo.
Hahahaha kwani wewe unatumia ID gani????
Mimi natumia jina langu la utani nilipewa JKT.Unataka nini tena????
mazagaone@ gmail.com
 
Serikali isilete mchezo kwenye hizi fani chemistry, biology na pharmacy hawa ndio wanaweza kugundua dawa wakiwezeshwa
Nini kilitabiriwa na nini kinatimia?
Nani anapingana na unabii?

Sent using Jamii Forums mobile app
. Kuna wenzako nao tangu miaka ya 80 kila tukio walikuwa wanasema maandiko yanatimia na huu ndio mwisho Mwana wa Adam yu aja.

Kumbukeni tangu Dunia hii miaka na miaka suala la magonjwa na Majanga vilikuwepo na vilipita kila kimoja kwa namna yake.
 
Mloganzila irudi iwe hospitali ya kufundisha wataalamu wa afya.
 
Nimefutilia mataifa mbalimbali kupitia mitandao naona madaktari na wakemia wakitaja dawa mbalimbali katika ugunduzi wa tiba ya Corona lakini Tanzania naona fofofo.

Sasa najiuliza pale Muhimbili University na Bugando mnajifunza kuosha vidonda tuu? Au ni vyuo vya ujenzi wa Maghorofa?

Hivi Tanzania tunasomesha wataalamu wa Afya au tunakaririsha watu jinsi ya kutoa dawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima watakuwa wanafanya utafiti wakigundua dawa watatangaza
 
Tanzania dawa hugunduliwa na waganga wa kienyeji. Wapo tu wanaumiza vichwa huku kila mmoja anaomba awe wa kwanza kugundua dawa apige hela.
Ndiyo waganga wetu
 

Attachments

  • IMG_20200328_202344.jpg
    IMG_20200328_202344.jpg
    18.2 KB · Views: 4
Kwanza Nikujuze ndugu mleta uzi ,Kinachotafutwa Ni Kinga na sio dawa...

Sasa nije kwenye swali kwamba Wataalam watanzania wako wapi wakati wenzao wa Nchi nyingine wakihangaiaka kutafuta suluhu ya Corona???

Wakati Fulani Swali Hujibiwa kwa Swali/Maswali ..

Hivyo basi, Tujiulize..

Je Tanzania imewahi kufanya Uwekezaji wowote serious kwenye Tafiti? Hasa katika kutenga Fungu la fedha kuwezesha watafiti??Kuna maazimio kadhaa yamewahi kuwekwa Kama vile kutenga 1% ya pato la Taifa iende kwenye Tafiti, Je limewahi kutekelezwa au iliishia kwenye makaratasi??

Je Tuna Maabara za viwango vya juu Kama hizo zinapofanywa Tafiti za Corona katika First World Countries?? Hapa Usisahau kuwa Maabara inayotumika kuthibitisha maambukizi ya Corona Ni moja tu Hadi Sasa Nchi nzima!

Katika Vipaumbele vya sekta ya Afya Tanzania na Nchi nyingine za Dunia ya tatu Kuna uwezekano wowote wa kutenga mabilioni ya Fedha kwenye kutengeneza "Facilities" kwaajili ya Tafiti Kama za Nchi ya Dunia ya Kwanza Huku wakati huohuo nchini mwao kukiwa na changamoto nyingine zenye ulazima zaidi Kama vifo vya kinama wajawazito, utapiamlo, upungufu wa vituo vya afya n.k ambazo zinademand fedha pia??????

Kwanini Wataalam wa Kiafrika hufanya makubwa Sana katika Nchi za Ulaya na America lakini katika Nchi zao hawafanyi lolote????



NB;
Sisi Kama Nchi tupambane na matatizo saizi yetu,kutokana na uwezo wa Facilities zetu na Nguvu zetu za kiuchumi..Hakuna namna tuanze kujenga First class Labs zitakazocost Billions wakati vitu vya msingi tu kama Utapiamlo na Udumavu kwetu Bado ni changamoto .It doesn't make sense .

"Rome wasn't built in a Day" hivyo hakuna muujiza utakaotokea ghafla bin vuu tuanze kushindana na Nchi Kama Marekani na Israeli kwenye Tafiti za kisayansi...

Wataalam wa Kitanzania na Afrika wana uwezo mkubwa kufanya hata zaidi ya hayo yanayofanywa na wenzetu..Tatizo ni mazingira..

Ili mbegu iote inahitaji vitu Kama maji/unyevu na mwanga kuota..

Ukiitupa mbegu Jangwani au Gizani Usitegemee au Usije kuiuliza mbegu baadae " Kwanini wewe hujaota wakati wenzio waliopo kandokando ya mto wanatoa matunda" ....








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia kuna Tafiti Nyingi tu zimefanywa na zinafanywa katika Vyuo husika ulivyovitaja na vingine vingi nchini, na baadhi hutangazwa..

Lakini Watanzania wako Interested na Ubuyu, Celebrities, Michezo, Umbea,Vituko na Matukio mengine yasiyo na Maana ..

Hata media zetu hazitoi Vipaumbele kwa habari Kama hizo Sababu haziuzi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kazi ya kuungana mataifaa na mataifa dacteri kwa dacteri alafu wewe ufanye iyo kazi pekeako na ukawa kimyaa bila kusema matumaini yako katika tafiti zako basi Tanzania kuna mafunzo ya ajabu sija pata kuona

Binafsi mimi ni mkemia,nipo nimejifungia naendelea na utafiti mkuu.
 
Jamn utafiti wa dawa na chanjo pia vunahitaji miundombinu, vifaa, fedha nk Sasa ndugu yangu hv km wenye nchi wapo kwenye kujifukiza na maombi wakiambiwa wa invest billions kwa ajili ya tafiti hzo itawezekana. N kuwaonea kwa kiasi flan
 
Back
Top Bottom