Wasomi wa kitanzania wanashindwa kwenda nje ya nchi kutafuta fursa mbalimbali kwasababu ya hivi vitu viwili(TOEFL na IELTS)

Una hoja nzuri ila sio sahihi kwa 100%

Sio kila scholarship inahitaji TOEFL/ IELTS hii ninakuhakikishia jaribu kufuatilia vizuri.

Njia nyingine ni sio lazima kufanya hiyo mitihani huwa kuna recommendation letters unaandikiwa na professors huwa wanahitaji walau wawili pia ikithibitisha English ilikua medium of instruction ulipokuwa chuoni.

Hata Nigeria yenye watu milioni 200+ kuna vyuo wanahitaji wapate score ya. walau 80 kwenye TOEFL

Nigeria kwa makadirio ina diaspora wapatao milioni 15 huku wengi wakiwa USA.

Nilijifunza kwa wanigeria walichonacho ni uthubutu ambao watanzania wengi hawana. Wanayo kampeni yao waniita "JAPA"

Maana ya neno hilo japa ni kutokomea/kukimbia kutoka katika hali usiyohitaji kwenye hili wapo serious sana na wanashikana mikono sana tofauti na diaspora wengine.

Pia fursa za kwenda nje zipo nyingi na tofauti kama ,visa sponsored jobs, exchange programmes pia unaweza kwenda kama mtalii ukifika unabadilisha status ya visa unapata na work permit.

Nchi zingine ambazo wanashikana mikono sana ni Wakenya na Wasomali , hawa ukienda jimbo la Minnesota [USA] ni rahisi kukutana na mkenya au msomali kama unavyoweza kuwa Eastleigh hapo Kenya.
 
Mwanangu Bufa, I mean braza Bufa safi sana.

Lazima watu watambue kuwa kimsingi wana jukumu. Yaani wananchi wanatakiwa kuwajibika kuijenga serikali. Na serikali ni watu haohao, kwa hiyo kimsingi ni kujijenga wao. Jukumu jukumu majukumu
 
Nimefanya utafiti ajua haitolewi na serikali ndio maana kuna sehemu nimependekeza serikali iweze kugharamia hizo ada kwa maslahi ya watu wake.
Serikali inafanya mambo ya kuijenga nchi

Sio ikafanye majukumu ya kuwapeleka wananchi wake kwenda kujenga nchi za nje tena kwa maslahi yao binafsi.

Yaani basically unataka kodi za wananchi ziwalipie hadi watakaotaka labda kwenda kula bata Dubai. Bora ingekuwa ni kula bata humuhumu nchini ili fedha zibaki ndani.

Kama ni binafsi utaamua basi jigharamie na hela utakazopata ni zako binafsi.
 

Hakuna fursa nchi za nje zaidi ya utumwa mamboleo! Ni akili iliyojifunga minyororo ya utumwa ndiyo inayowaza kwenda nje ya nchi. Wazungu wenyewe hadi wanachapana risasi kwa sababu ya msongo wa maisha wewe unawaza kwenda nje! Ni ujinga mtupu na umasikini wa fikra! Hakuna bara zuri kwa kuishi kama Africa! Huko mnaenda kuchanganyikiwa tu na kurudi huku mkiwa maskini wa kutupwa!
 
Bado hujajua...angalau una mwanga kwa mbali.
 
Ukishindwa kufanya TOEFL kwa sababu hizi hata huko nje hujastahili kwenda.

You are simply not resourceful enough.

Kama umeshindwa kutoka Kigoma kuja Dar kufanya TOEFL, utawezaje kutoka Dar kwenda Los Angeles, USA?
 
Wakati wa Moi Kenya iliwapa mchongo wauguzi kwenda Marekani.....Leo wakenya wengi wanamiliki majumba ya kutunza wazee huko Marekani na fedha wanazotuma nyumbani kwa mwaka ni billions Ksh......jaribu kutafakari.
 
Hili ni suala la mtu binafsi. Uamuzi wa wapi panafaa unategemea mambo mengi sana tofauti.

Na ukisikia mtu anakuwa absolute "nje ni hivi, nyumbani ni hivi" basi ujue huyo ni mjinga asiyejua umuhimu wa nuance.

Ana generalize kijinga jambo lenye nuance nyingi sana.
 
Huo ndio ukweli.Angalia wanaojiita maprofessor na Viongozi wa Serikali wanaongea Kiingereza Cha hivyo kabisa na hakina Grammer.

Wengine dizaini ya kina Ndalichako wamesoma na kuishi Nje ila Bado zero kabisa kwenye lugha.
 
Wakati wa Moi Kenya iliwapa mchongo wauguzi kwenda Marekani.....Leo wakenya wengi wanamiliki majumba ya kutunza wazee huko Marekani na fedha wanazotuma nyumbani kwa mwaka ni billions Ksh......jaribu kutafakari.
It makes no sense

Mtu awe nje anafanya kazi halafu atume Ksh.

Fuatilia vizuri
 
Sioni kama hilo limekaa sawa kwa kudhani kwamba ili uende nje unatakiwa ujue kiingereza. Vipi kama naenda nchi ambayo ni non English speaking, bado nahitaji hicho kiingereza? Na tatizo la wahitimu wa Tanzania sio kutomaster lugha bali wana shallow mentality inayochagizwa na poor system of education and it's materials.
 
Ni ukweli kabisa usiopingika kwamba bara la Afrika kwa asili ni mahali pazuri sana pa kuishi hapa duniani, TATIZO KUBWA zaidi linalofanya bara hili la Afrika kuonekana kuwa ni mahali pabaya pasipofaa watu kuishi kwa amani ni kutokana na kuwepo kwa TAWALA MBAYA ZISIZOFAA kwenye hizi nchi zetu.
Tawala zilizopo ktk nchi za Afrika hazina mvuto kabisa wa kuweza kuwafanya watu kuwa na amani na furaha ya kuendelea kubaki ktk ardhi ya Afrika.
 

Basi toeni ujinga huo msiulete humu. Ukitaka kwenda nenda wewe na kama kiingereza hakipandi ni juu yako wewe, utabaki unahangaika na kwenda nje hadi unaota mvi na umo humu humu! Ulidhani huko nje kuna mjomba wako huko! Huko ni kula mijeledi tu bila hata kupata usingizi kijana! Wewe nenda kalime tu!
 
Ujinga ni kuniambia mimi "toeni ujinga huo msituletee humu" wakati mimi sina mshirika hapa na wala sijaleta mada.
 
Asante kwa kuendelea kutufungua
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Sikia wewe ..ni hivi hii serikali yako haina uwezo wa kutumia rasilimali watu ni bora wafunguliwe milango wakatumiwe na mataifa mengine ..kutoka huko watapata pesa na watawekeza katika nchi yao,pia watapata ujuzi wa mambo mbalimbali ambapo watakuja kusaidia nchi yao katika nyanja mbalimbali..we have to think beyond the the box...watanzania wengi reason capacity ipo chini mnoo..ndio maana ni masikini na huku wana rasilimali za kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…