Wasomi wa SUA wanalisaidia nini Taifa?

Wanapambania matumbo Yao
 
Malalamiko mengi uliyoongea yanatatuliwa kisera zaidi.
 
Binafsi ni mhitimu wa SUA BSc in Agricultural Engineering ila mpaka sasa sijalisaidia chochote taifa hili kupitia elimu hii niliyoipata.
Nipo kwenye mchakato wa kuangalia namna ya kulisaidia ila ngojeni kwanza nikomae kutafuta hela ya kula mtaani nikiipata ntarudi kulisaidia,maana ajira hazipo
 
Kama makubwa si uyataje?
Ukijumlisha ngano pamoja na mafuta
 
Tatizo ni wasomi waliosoma Engineering UDSM wameshindwa kutengeneza hata Trekta moja kiasi kutufanya sisi tuosoma SUA kuendelea kulima kwa Jembe la mkono baada kumaliza chuo
 
Wasomi wa Kibongo ni sawa na Steve Nyerere tu....hawana weledi, wao kazi kupiga kelele tu ili wasikike lakini hawana lolote. Sijawahi sikia msomi wa UDSM au Muhimbili amefanya la maana hapa nchini zaidi ya kuongea broken English muda wote na kujifanya hajuwi lugha yake mama (Kiswahili).
 
Mtajiju, sisi tumepata GPA kali tunafundisha Vyuo, na leo tupo tunkula bata club, na salale i.etoka tangu juz,
Manyoko!
 
Wamekuwa wanafundisha kilimo Cha matikiti na maparachichi na vanilla wanasema zinalipa sana.
 
Si wasomi wa SUA tu, vipi wana sayansi wetu wanafanya nini cha maana?
 
Acha liajiri tu kiduchu hawana msaada wowote kwa taifa naona wanaleta hasara tu
Ulitaka wafanye nini kwa mfano? Unafikri hakuna mbegu walizotafiti kwa ajili ya nchi yetu? Usiwalinganishe na wale wa Jalalani ambao wanaishia kutoa ripoti za kinyesi na mikojo!
 
Hizo mbegu unatumia unafikri zimefanyiwa utafiti na darasa la saba?
 
Ngano imetoka 1200 kwa sasa ni 2000, sababu tunaagiza nnje na huko nnje vita ya urusi na Ukraine ni sababu moja wapo maana inasemekana wanazalisha ngano kwa kiasi kikubwa kwa sasa hawauzi popote kwasababu ya vita na vikwazo alivyowekewa Urusi
Majibu kwa baadhi ya maswali yako unayo mwenyewe lakini bado unawalaumu wataalamu wa SUA? You cant be serious dude!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…