Wasomi wote wasio na ajira Tanzania kazanieni wazazi wenu walioko kwenye ajira walipwe mshahara mzuri na wachukue mafao yanayopatikana baada ya miaka

Wasomi wote wasio na ajira Tanzania kazanieni wazazi wenu walioko kwenye ajira walipwe mshahara mzuri na wachukue mafao yanayopatikana baada ya miaka

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wakuu

Hili ni bandiko la ushauri kwa vijana wasio na ajira lakini pia kwa mamlaka za ajira

1. Vijana wote wapaaze sauti kwa mamlaka na bunge kubadilisha sheria zinazopanga mishahara yenye ulali sawa kuelekea ukoma wa umri elekezi wa kustaafu (55) na wa lazima (60) ili wanapotoka wasiwe tegemezi
2. Mchangiaji yeyote katika mifuko ya jamii anapozidi utumishi wa miaka kumi mfululizo ni busara kwa miaka inayoongezeka michango yake anapoihitaji kuichukue sheria iruhusu ili kumfanya ajiandae vyema kung'atuka ili awaachie vijana ajira hiyo
3. Michango ya mchangiaji yeyote inatakiwa iwe na faida kwake badala ya riba ya asilimia 2 (2%) kwa mwaka wakati serikali inapowekeza kwenye miradi inahipatia faida kubwa ambayo baadhi yake inaishia kwenye mikono isiyo salama ya watumishi wasio waaminifu. Riba ipandishwe hadi asilimia 12 (12%) ili kuendana na wakati wa thamini ya fedha kushuka
 
Back
Top Bottom