Wassira: Hati ya Muungano imesha fika Dodoma leo!

Wassira: Hati ya Muungano imesha fika Dodoma leo!

mNaz

Senior Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
104
Reaction score
31
Baada ya mh. Wassira kutoa kauli na kuwahakikishia watanzania kuwa hati ya muungano ipo na ataiwasilisha ndani ya siku mbili.

Taarifa zenye uhakika kabisa kuwa hati imeshawasili Dodoma kwa maana ya nakala/copy na asubuhi itawasilishwa nakala iliyothibitishwa/certified true copy na kila mjumbe wa bunge la katiba atapewa nakala yake kama kumbukumbu.
 
Baada ya mhe wasira kutoa kauli na kuwa akikishia watanzania kuwa hati ya muungano ipo na ataiwasilisha ndani ya siku mbili taarifa zenye uwakika kabisa kuwa hati imesha wasili dodoma kwa maana ya nakala/copy na asubuhii itawasilishwa nakala iliyodhibitishwa/certified true copy na kila mjumbe wa bunge la katiba atapewa nakala yake kama kumbukumbu.

Inatia wasiwasi!

Hii hati imekuwa mana ionekane kwa msimu? Ni juzi tu ilikuwa haipo! Mara ikawa UN! mara imetokea ghafla!

Kwa hiyo baada ya kuumbuliwa haikupelekwa UN ndo imepatikana ? Kama iliwahi kuhitajiwa mpaka na mahakama na bado haikupelekwa ilikuwepo hiyo? Na ilikuwa wapi kuletwa mapema pale ilipokuwa inahitajiwa na wabunge kwa ajili ya uthibitisho?

Hii ni serikali ya ovyo na imezoea uhuni. Msinilaumu kwa kutokuwa na imani na hati hiyo. mazingira yanatia shaka.
 
Mara ika faxiwa toka sehemu moja kwenda nyingine mnamo tarehe 14 April, 2013; kaaazi kweli kweli.
 
Mara ika faxiwa toka sehemu moja kwenda nyingine mnamo tarehe 14 April, 2013; kaaazi kweli kweli.
attachment.php
 
Wote mlio changia hapo juu mnajikuta mnaleta umbea tu. Subirini tupewe hati tutaichunguza baada ya kupewa. Na mnaobeza na kusema feki kwani origina mkonayo na kama mnayo wasilisheni..... wasira a.k.a SIMBA WA YUDA.
 
Uwezekano wa kuchakachua ni mkubwa! Any way, tanganyika irudi kwanza, muungano baada ya tanganyika kufufuliwa!
 
Wakati mwingine tuwe na heshima kwa viongozi waliotuongoza miaka ya zamani ambapo hapakuwa na komputa. Kudai kuwa viongozi wa Zanzibar wote waliotumikia serikali ya Nyerere, hasa wale wa kwanza kutoka kwenye baraza la mapinduzi akina Babu, Jumbe, Hanga, Karume, Moyo na wengine walikuwa ni wajinga sana kutumikia serikali ya Muungano ambao hawakuwa wameuafiki kweli ni kuwadhalilisha sana viongozi hao ambao wengi wao wameshatangulia mbele ya haki.

Ni afadhali tujadiliane kuwa Muungano huu ambao wazee wetu waliafikiana wakati huo sisi hatuuhitaji leo kwa hiyo tuachane nao kuliko kuelata maswali yasiyo kuwa na maana kama vile hati ya muungano ina walakini, sahihi haikukaaa sawa na upuuzi wa namna hiyo tuachane na hayo tuangalie tu kama Muungano kweli unatufaa. Mimi sasa hivi nina imani kabisa kuwa Muungano huo hautufai tena, ndiyo maana ninapenda kuona Tanganyika inarudi tena. Wenzetu waliahi kusema kuwa "you don't know its value until you miss it." Nitakapo-miss muungano labda ndipo nitajiangalia tena ila kwa sasa nasema "enough is enough" Muungano huu uvunjwe. Nchi yenyewe imekuwa haina mwelekeo tena kwa hiyo ni afadhali tuanze upya tu.
 
Inatia wasiwasi!

Hii hati imekuwa mana ionekane kwa msimu? Ni juzi tu ilikuwa haipo! Mara ikawa UN! mara imetokea ghafla!

Kwa hiyo baada ya kuumbuliwa haikupelekwa UN ndo imepatikana ? Kama iliwahi kuhitajiwa mpaka na mahakama na bado haikupelekwa ilikuwepo hiyo? Na ilikuwa wapi kuletwa mapema pale ilipokuwa inahitajiwa na wabunge kwa ajili ya uthibitisho?

Hii ni serikali ya ovyo na imezoea uhuni. Msinilaumu kwa kutokuwa na imani na hati hiyo. mazingira yanatia shaka.

Nakubaliana na wewe.
 
Ukienda kwenye tovuti ya bunge ambako walifanya project ya kuscan documents zote za bunge na kuziweka online, kuna zile ambapo sahihi ilikuwa imeshafifia wakawa wanaiongozea wenyewe. Kufanya hivyo hakukuwa na maana kuwa sheria ile siyo halali tena. Kuna zile walizotumia optical character recognition zikawa zinasomeka kiajabu ajabu; hata hivyo originals lazima ziwe zimetunzwa.

Nyerere alikuwa anatumia sana karamu ya kijani, wino wa kuchovya ambao baada ya muda unaweza kupauka iwapo karatasi haikuhifadhiwa vizuri.
 
Muda wote inauliziwa hiyo hati ilikuwa iko wapi??
Au ilikuwa hm kwa Wassira??
 
Huo sasa ni utoto na ujinga wanafanya
 
Back
Top Bottom