Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WanaJF wenzangu naomba tutafakari kwa makini juu ya tukio hili la suala la Hati ya Muungano Katika taratibu za uwekaji wa Saini nyaraka muhimu uwa lazima zisainiwe nyaraka zaidi ya moja ili kila upande unaohusika uweze kuwa na nyaraka yake. kwa hiyo katika nyaraka hii yaani HATI YA MUUNGANO ni lazima zilisainiwa HATI zaidi ya 3 yaani moja ilitakiwa iwepo kama kumbukumbu ya Serikali ya Tanganyika, Nyingine Serikali ya Zanzibar na nyingine UN na moja kuwepo kwenye hii serikali ya Muungano. Tumeweza kuonyeshwa hiyo moja je hizi zingine ziko wapi tunaomba tuonyeshwe ili tujiridhishe uhalali wa hii iliyopo.
Tukiwabana sana, mwisho wa siku watatuambia kwamba, hati ya muungano ni ule udongo aliouchanganya Nyerere peke yake!~
Ziko mbili, Hati yenyewe imesema "signed in duplicate."kwani zipo ,,ngapi?
Na nchi zipo ngapi?
Wote mlio changia hapo juu mnajikuta mnaleta umbea tu. Subirini tupewe hati tutaichunguza baada ya kupewa. Na mnaobeza na kusema feki kwani origina mkonayo na kama mnayo wasilisheni..... wasira a.k.a SIMBA WA YUDA.
Serikali mbili HAZIKUBALIKI!
MTANGANYIKA DAIMA!
Tukiwabana sana, mwisho wa siku watatuambia kwamba, hati ya muungano ni ule udongo aliouchanganya Nyerere peke yake!~
Baada ya mh. Wassira kutoa kauli na kuwahakikishia watanzania kuwa hati ya muungano ipo na ataiwasilisha ndani ya siku mbili.
Taarifa zenye uhakika kabisa kuwa hati imeshawasili Dodoma kwa maana ya nakala/copy na asubuhi itawasilishwa nakala iliyothibitishwa/certified true copy na kila mjumbe wa bunge la katiba atapewa nakala yake kama kumbukumbu.
Alikuwa baba wa TaifaKwa nn Nyerere alikamata zile chupa peke yake?