Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Wakati mwingine tuwe na heshima kwa viongozi waliotuongoza miaka ya zamani ambapo hapakuwa na komputa. Kudai kuwa viongozi wa Zanzibar wote waliotumikia serikali ya Nyerere, hasa wale wa kwanza kutoka kwenye baraza la mapinduzi akina Babu, Jumbe, Hanga, Karume, Moyo na wengine walikuwa ni wajinga sana kutumikia serikali ya Muungano ambao hawakuwa wameuafiki kweli ni kuwadhalilisha sana viongozi hao ambao wengi wao wameshatangulia mbele ya haki.
Ni afadhali tujadiliane kuwa Muungano huu ambao wazee wetu waliafikiana wakati huo sisi hatuuhitaji leo kwa hiyo tuachane nao kuliko kuelata maswali yasiyo kuwa na maana kama vile hati ya muungano ina walakini, sahihi haikukaaa sawa na upuuzi wa namna hiyo tuachane na hayo tuangalie tu kama Muungano kweli unatufaa. Mimi sasa hivi nina imani kabisa kuwa Muungano huo hautufai tena, ndiyo maana ninapenda kuona Tanganyika inarudi tena. Wenzetu waliahi kusema kuwa "you don't know its value until you miss it." Nitakapo-miss muungano labda ndipo nitajiangalia tena ila kwa sasa nasema "enough is enough" Muungano huu uvunjwe. Nchi yenyewe imekuwa haina mwelekeo tena kwa hiyo ni afadhali tuanze upya tu.
Hatuwezi kufikia kuamua kuuvunja muungano, bila kukiri kuwa makubaliano yaliyofanywa yalikuwa na kasoro. Kadhalika , hatuwezi kukubali kasoro zilizokuwepo halafu tukajifanya hatujui waliozisababisha. Hii ndiyo maana kila siku napiga kelelele humu kwa watu kuacha ushabiki wa kipuuzi na kuangalia ni hoja ipi ina ukweli na ni ipi inabeba maslahi ya nchi, na siyo hoja ipi imesemwa na nani na kama ni mCCM au mCHADEMA! Ni kwa sababu historia ndivyo inavyoandikwa. Kwa hiyo pale ambapo viongozi wetu tuliowachagua waliandikisha historia ya ovyo kabisa, ni vizuri tukakiri hilo, bila kigugumizi wala kupepesa macho.Na historia ituhukumu hivyo, kuwa sisi, baada ya kuangalia na kutafakari kwa kina, tuligundua kuwa viongozi wetu walifanya jambo la ovyo kabisa. Halafu tuwaambie watoto wetu ni kipi kilikosewa ili wao wapate kurekebisha. Vinginevyo kugundua makosa na kuendelea kuyapaka mafuta, ni kuhalalisha watoto na wajukuu zetu (taifa la kesho) kuishi kwenye uwongo ulioanzishwa na hao marehemu, ambapo tutakuwa hatuna tofauti nao kama tutashindwa kusema hilo lina makosa.
Kuhusu kuuvunja au kuunusuru, mimi nadhani ni mapema kufika huko. Kwanza tuone uhalali wa makubaliano yale, halafu tuone kama bado tuna sababu (kwa leo) za kuwa na makubaliano ya aina hiyo. Kisha kama tutaona inafaa tuendelee au kama haifai turekebishe makubaliano au kama haiwezekani basi tuuvunje! hili ni swala linalohitaji maamuzi ya wananchi wenyewe, na siyo viongozi kuamua kama walivyofanya kipindi kile na kama ambavyo wanalazimisha kufanya leo!