Wakati mwingine tuwe na heshima kwa viongozi waliotuongoza miaka ya zamani ambapo hapakuwa na komputa. Kudai kuwa viongozi wa Zanzibar wote waliotumikia serikali ya Nyerere, hasa wale wa kwanza kutoka kwenye baraza la mapinduzi akina Babu, Jumbe, Hanga, Karume, Moyo na wengine walikuwa ni wajinga sana kutumikia serikali ya Muungano ambao hawakuwa wameuafiki kweli ni kuwadhalilisha sana viongozi hao ambao wengi wao wameshatangulia mbele ya haki.
Ni afadhali tujadiliane kuwa Muungano huu ambao wazee wetu waliafikiana wakati huo sisi hatuuhitaji leo kwa hiyo tuachane nao kuliko kuelata maswali yasiyo kuwa na maana kama vile hati ya muungano ina walakini, sahihi haikukaaa sawa na upuuzi wa namna hiyo tuachane na hayo tuangalie tu kama Muungano kweli unatufaa. Mimi sasa hivi nina imani kabisa kuwa Muungano huo hautufai tena, ndiyo maana ninapenda kuona Tanganyika inarudi tena. Wenzetu waliahi kusema kuwa "you don't know its value until you miss it." Nitakapo-miss muungano labda ndipo nitajiangalia tena ila kwa sasa nasema "enough is enough" Muungano huu uvunjwe. Nchi yenyewe imekuwa haina mwelekeo tena kwa hiyo ni afadhali tuanze upya tu.