Wassira: Ieleweke wazi tunapoandika Katiba Mpya Sera ya CCM ni Serikali 2 kuelekea 1 na Siyo vinginevyo

Amesema sera ya chama, nami naamini hivo kuwa ata iweje CCM hawawezi kukubali serikali 3
Sera za vyama ndiyo zinatakiwa zikidhi matakwa ya Kikatiba syo Katiba ikidhi Sera ya chama cha siasa,Katiba siyo mali ya CCM, kauli ya Wasira ni uchochezi dhidi ya wananchi ambao ndiyo waliotoa maoni ya kuwa na Serikali tatu. Watu aina ya Wasira ni hatari kwa usalama na ustawi wa nchi.
 
Mzee Wassira kupitia mahojiano maalum yaliyofanywa na TBC yakimuhusisha pia Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema Sera ya CCM kuhusu muundo wa Serikali haitabadilika.

Wassira amemwambia Zitto Kabwe kwamba Ukitaka Serikali 3 ujue hakuna Katiba Mpya itakayopatikana.

Ukweli Mchungu!
Misimamo ya wahafidhina ndani ya chama kama hawa ni ya hovyo kabisa, pengine angevuta subira ili mchakato uanze rasmi ndipo kisha aanike kile kilichopo akilini mwake. Ni misimamo kama hii ambayo ilikwamisha Bunge la Katiba ili kutupatia wananchi Katiba mpya.

Angalisubiri muda sahihi wa kuanza kufanya 'political manipulation" kuliko kuanza mapema kabisa na aina hii "preconceived notion" zenye kila dalili ya kutaka ku-influence matakwa binafsi. Busara humtuma mtu kufanya jambo sahihi katika muda sahihi.
 
Hili nimewaambia sana chadema alikini hawasikii
 
Mzee Wassira kupitia mahojiano maalum yaliyofanywa na TBC yakimuhusisha pia Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema Sera ya CCM kuhusu muundo wa Serikali haitabadilika.

Wassira amemwambia Zitto Kabwe kwamba Ukitaka Serikali 3 ujue hakuna Katiba Mpya itakayopatikana.

Ukweli Mchungu!
🤣🤣🤣
 
Huo ndo msimamo wa CCM. PINDA na WASIRA ndo think tanks wa CCM ktk suala la KATIBA mpya.

Anyway tutawakumbusha kuwa Mzee Warioba Si mwana CDM, ni CCM mwenzao.

Baada ya kupewa KAZI Kwa maslah ya umma, alikusanya maoni na WANANCHI ndo walipendekeza Serikali tatu.

Vita hii WANANCHI tutashinda, haitoahirishwa mechi Wala hakuna Suluhu.
Acha kudanganya watu. Hayo maoni yalipigiwa kura au referendum?. Mpaka uka conclude kwamba yalikuwa mapendekezo ya wengi zaidi?. Umuhimu wa katiba upo palepale lkn muda ukifika ndio utapata nafasi ya kupigia debe msimamo wako. Kwa sasa unatudanganya mkui
 
NIMEPENDA UKWELI WA MZEE WETU WASSIRA, NA HUO NDIO UKWELI WENYEWE. SEREKALI TATU ITAHARIBU UMOJA WETU ADHIMU, TUWE MAKINI, KATIKA KUULINDA MUUNGANO WETU, MUUNGANO NI BORA KULIKO CHOCHOTE KILE.
 
Tatizo Wazanzibar hawajitambui, vinginevyo wangeshajitafutia uhuru wake
Hakuna wa kuuvunja muungano Amini hilo,ni bora sote tufe kuliko muungano kuvunjika!, na tutaupigania kwa jasho na damu na kuulinda usivunjike!
 
Kwani tunatengeneza katiba ya CCM au Katiba ya Tanzania?
Kwani sera za vyama huwa ni misahafu isiyobadilika?
Kwani Katiba yote inahusu muundo wa serikali za muungano tu?

Sera za CCM ziko kwa ajili ya wanaCCM tu (hutungwa na kupendekezwa na wanachama wa CCM tu), hazituhusu watanzania wote. Katiba ni jambo la watanzania wote, na watanzania wengi sio wanachama wa vyama vyovyote vya siasa.
 
Mzee Wassira kupitia mahojiano maalum yaliyofanywa na TBC yakimuhusisha pia Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema Sera ya CCM kuhusu muundo wa Serikali haitabadilika.

Wassira amemwambia Zitto Kabwe kwamba Ukitaka Serikali 3 ujue hakuna Katiba Mpya itakayopatikana.

Ukweli Mchungu!
Nafikiri kuna haja ya kufahamu.
Hatuhitaji katiba ya ccm wala chadema, wakati tume zote zinaundwa kukusanya maoni zimekuwa zikileta maoni ya wananchi siyo maoni ya chama fulani.
Wananchi hawajasema ccm ibadili sera yake wala chadema au ACT ibadili sera yake bali sisi wananchi ndio tunaotaka, sasa ukiona mtu anasema " ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" kwa maoni yangu sidhani kama huyu mtu anafahamu kama nchi si mali ya chama fulani. Na pia tupunguze ukali wa maneno ili tujenge nchi yetu" kusema ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" ni kujisahau kama kwamba nchi hii iko mfukoni kwako unachotaka wewe ndicho lazima kifanyike, tusijisahau kiasi hicho.
 
NIMEPENDA UKWELI WA MZEE WETU WASSIRA, NA HUO NDIO UKWELI WENYEWE. SEREKALI TATU ITAHARIBU UMOJA WETU ADHIMU, TUWE MAKINI, KATIKA KUULINDA MUUNGANO WETU, MUUNGANO NI BORA KULIKO CHOCHOTE KILE.
Hoja yako haina mantiki kabisa.
Kivipi serikali tatu zitaharibu umoja wetu badala ya kuuimarisha?
Kama kuwa na serikali nyingi(tatu) ni tatizo, kwanini usije na hoja ya kutaka kuwa na serikali moja badala ya mbili?
 
Misimamo ya wahafidhina ndani ya chama kama hawa ni ya hovyo kabisa, pengine angevuta subira ili mchakato uanze rasmi ndipo kisha aanike kile kilichopo akilini mwake. Ni misimamo kama hii ambayo ilikwamisha Bunge la Katiba ili kutupatia wananchi Katiba mpya.

Angalisubiri muda sahihi wa kuanza kufanya 'political manipulation" kuliko kuanza mapema kabisa na aina hii "preconceived notion" zenye kila dalili ya kutaka ku-influence matakwa binafsi. Busara humtuma mtu kufanya jambo sahihi katika muda sahihi.
Ni bora ametamka mapema watu watakuwa wanajua kumbe wahafidhina wa namna yake ndio waliokwamisha ile Rasimu ya Warioba na kwamba mara hii njia gani itumike ili mambo yasijirudie ya kupoteza pesa za kodi ya wananchi kwa kuwalipa wajumbe kama ilivyokuwa kwa JK !!
 
Nafikiri kuna haja ya kufahamu.
Hatuhitaji katiba ya ccm wala chadema, wakati tume zote zinaundwa kukusanya maoni zimekuwa zikileta maoni ya wananchi siyo maoni ya chama fulani.
Wananchi hawajasema ccm ibadili sera yake wala chadema au ACT ibadili sera yake bali sisi wananchi ndio tunaotaka, sasa ukiona mtu anasema " ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" kwa maoni yangu sidhani kama huyu mtu anafahamu kama nchi si mali ya chama fulani. Na pia tupunguze ukali wa maneno ili tujenge nchi yetu" kusema ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" ni kujisahau kama kwamba nchi hii iko mfukoni kwako unachotaka wewe ndicho lazima kifanyike, tusijisahau kiasi hicho.
Kwani mchakato wa Katiba mpya unaendeshwa na hao Wananchi?!
 
Mzee Wassira kupitia mahojiano maalum yaliyofanywa na TBC yakimuhusisha pia Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema Sera ya CCM kuhusu muundo wa Serikali haitabadilika.

Wassira amemwambia Zitto Kabwe kwamba Ukitaka Serikali 3 ujue hakuna Katiba Mpya itakayopatikana.

Ukweli Mchungu!
Haya maneno ya mzee Wassira si ya kuyabeza hata kidogo, yanaitaji kuyatafakari sana kwani yanaweza yakawa ndio mwisho wa mchezo wa takwa la katiba mpya

Tujiulize aliyoyasema mzee wassira ndio kweli takwa kuu la ccm??

Je wapi kuna huraisi kati ya upatikanaji wa serikali moja au serikali tatu??

Je Zanzibar watakubali kuwa na serikali moja??

Hapa pana mtego na kama kweli tunataka katiba mpya basi akili kubwa sana inaitajika
 
Haya maneno ya mzee Wassira si ya kuyabeza hata kidoga, yanaitaji kuyatafakari sana kwani yanaweza yakawa ndio mwisho wa mchezo wa takwa la katiba mpya

Tujiulize aliyoyasema mzee wassira ndio kweli takwa kuu la ccm??

Je wapi kuna huraisi kati ya upatikanaji wa serikali moja au serikali tatu??

Je Zanzibar watakubali kuwa na serikali moja??

Hapa pana mtego na kama kweli tunataka katiba mpya basi akili kibwa sana inaitajika
Hili la Wassira ndilo lingeweza kuja kuharibu mchakato wote wa kupatikana katiba mpya kama hilo lingeibuliwa katikati ya mchakato !! Lakini kwa kuwa wahafidhina wamejichanganya na kuliibua kabla ya mchakato wenyewe kuanza watu wa namna yake wasipewe nafasi !!
 
Sasa ndio ameshalileta kabla ya mchakato kuanza. Tuna majibu gani ktk hili suala
 
Wameanza tena hoja kuu za wanasiasa wa Tanzania ni CCM serikali mbili na Chadema tatu , CCM muungano ni legitimacy chademo hamaamini, soon utasikia wakibishania hati za muungano na madaraka ya Rais, Tanzania tuna wanasiasa wa hovyo sana hawa hawa wapinzani uchwara

USSR
Hujawahi kumiliki akili Kwa hiyo hatukushangai. Hata ukisoma ulichoandika wewe mwenyewe hutakielewa.
 
Back
Top Bottom