Nafikiri kuna haja ya kufahamu.
Hatuhitaji katiba ya ccm wala chadema, wakati tume zote zinaundwa kukusanya maoni zimekuwa zikileta maoni ya wananchi siyo maoni ya chama fulani.
Wananchi hawajasema ccm ibadili sera yake wala chadema au ACT ibadili sera yake bali sisi wananchi ndio tunaotaka, sasa ukiona mtu anasema " ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" kwa maoni yangu sidhani kama huyu mtu anafahamu kama nchi si mali ya chama fulani. Na pia tupunguze ukali wa maneno ili tujenge nchi yetu" kusema ukitaka serikali tatu ujuwe hakuna katiba" ni kujisahau kama kwamba nchi hii iko mfukoni kwako unachotaka wewe ndicho lazima kifanyike, tusijisahau kiasi hicho.