Wastani wa ufaulu shule Binafsi unaumiza

mzamifu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2010
Posts
6,400
Reaction score
3,853
Shule za binafsi huweka wastani wa alama za ufaulu ili mtoto aweze kuendelea na masomo. Shule moja hapa Dar imeweka wastani wa alama 61. sasa mtoto mmoja kapata wastani alama 59 tena kwa kujipinda hasa.

Lakini shule imemlazimisha kurudia kidato. mtoto kaumia hasa hana raha kabisa.

Hili tatizo lianaweza kutatuliwaje?
 
mzamifu

Kama kajipinda kisawa sawa na kapata 59 huyo ni hard learner hizo shule hazimfai, zinataka wanajua hawafundishi mtoto kujua.
 
Last edited by a moderator:
Kama kajipinda kisawa sawa na kapata 59 huyo ni hard learner hizo shule hazimfai, zinataka wanajua hawafundishi mtoto kujua

Nimekuelewa mkuu, ila inawaumiza watoto kisaikolojia. pengine inaweza kumboma badala ya kumjenga. Shule zinajengwa kwa msingi wa sifa ili ku attract wenye fedha lakini kwa bahati mbaya si wote wenye pesa wanazaa ma genius.
 
Ahame..
Masharti na vigezo kuzingatiwa
Hilo ni suluhisho mojawapo. lakini kitendo cha kuhama huku akikjua kashindwa ndo kuumia kwenyewe.
 
Kama taifa na kama taasisi ni lazima tujifunze kujiwekea malengo na kuyafikia; mambo ya bora liende hayatatufikisha popote na kimsingi taifa limekwama kwa sababu ya bora liende.

Kama vipi mpeleke mwanao al-mujahideen seminary ambao kwao hata wastano wa 0 sio issue sio lazima ung'ang'anie zenye malengo wakati mwanao kilaza.
 
Kusoma kwa bidii sana, na miguu aweke kwenye ndoo ya maji.
 
Wewe hamisha tu maana hata hapo tayari ameshayumba. Kwa hiyo ungependa kusiwe na wastani wa ufaulu ili woye wawe wanapita?
hilo la kuhamisha sawa kuliko kurudia
 
si kilaza as such ila alikuwa na tatizo muda wa maandalizi
 
Wandugu baada ya hii michango michache nimegundua Watanzania wanapenda viwango. Bila shaka shule za serikali zingeweka viwango japo 40 kwa uchache wanafunzi na wazazi wangejitahidi zaidi na elimu ingekuwa bora zaidi.

Kwa sasa kiwango cha kufaulu mfano form 2 kwenda form 3 ni wastani wa alama 20 tu! kutoka alama 30 za awali.
 
Arudie tu baba si ameashindwa kwan hakuna walio faulu?
 
Nakumbuka hivi karibuni limetolew agizo na Mheshimiwa Waziri Kassim Majaliwa, kuwa ni marufuku kwa shule binafsi kuwarudisha wanafunzi warudie darasa kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu.

Sasa sielewi agizo hili ni kwa shule za msingi na sekondari za binafsi ama laah?
 
Nimekuelewa mkuu, ila inawaumiza watoto kisaikolojia. pengine inaweza kumboma badala ya kumjenga. Shule zinajengwa kwa msingi wa sifa ili ku attract wenye fedha lakini kwa bahati mbaya si wote wenye pesa wanazaa ma genius.

unachosema ni kweli kuna shule inaitwa nyakahoja huku mwanza huwezi jua wanataka nini hasa. kuna mtoto amepata 92% kwenye mtihani wa kujiunga kawekwa reserve list.
 
Hakuna shule isiyokuwa na viwango mpaka vyuo vikuu. Hivyo viwango ni sehemu ya kujifunza kuweka malengo ya juu na kuyafikia. Halafu wewe mwenyewe unasema alikuwa na matatizo kwenye kujiandaa then unalalamika nini sasa!

Naamini huo wastani ni wa masomo yote ukichanganya na assessments. Kuna watu wamesoma kwenye shule zenye viwango kama hicho na wamefaulu na wengine waliondoka na kujiunga na shule zenye viwango vya chini ya hapo.
 
Agizo la kutokufikiria hilo, na shule binafsi wamelikataa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…