Wastara alizwa mamilioni ya pesa na wachina

Wastara alizwa mamilioni ya pesa na wachina



Muigizaji maarufu wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ametapeliwa mamilioni ya fedha na kampuni moja ya simu ya Wachina baada ya kuingia nao mkataba wa kuwa balozi wao hapa nchini.
Wastara aliingia mkataba na Wachina hao mwaka jana ambapo alitakiwa awe analipwa shilingi milioni 400 kwa kila mwaka lakini ghafla Wachina hao wakaingia mitini.


“Pesa ambayo nawadai ni kama milioni 84. Kabla ya wao kuja nchini walitaka nianze kutumia pesa zangu kuandaa tisheti, kofia na mambo mengine ya kipromosheni. Kila nikiuliza kwamba mbona simu zenyewe haziji, maelezo yakawa kwamba wameagiza mzigo nje ya nchi, walipoona nawasumbua wakaingia mitini.

“Ilipopita miezi mitatu bila kuona maendeleo yoyote nilianza kuwasiliana nao tena, wakaanza kuniletea Kiswahili kingi, nikashtuka na kuweka mwanasheria wangu amba ambaye alikuwa nao sambamba, napo wakajaribu kumnyamazisha kwa pesa wakashindwa,” alisema Wastara.

Akaongeza kuwa, mara ya mwisho walikwenda kwenye kikao cha kujua hatima ya malipo yake na kinachoendelea ndipo afisa masoko wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Raymond Kalika alipomwambia kuwa Wachina hao wamerudi kwao.

“Yaani nahitaji msaada wa serikali ili nipate pesa zangu,hawawezi kunidhulumu kiasi chote hicho cha pesa katika kipindi kigumu kama hiki,” alisema Wastara.

Raymond ambaye ndiye aliyemuunganisha Wastara na Wachina hao alipoulizwa juu ya suala hili alijibu kwa kifupi:

“Ukweli wote nimeshamwambia Wastara, hapa tunasubiri hatua zifuatwe, siwezi kuwa na maongezi zaidi ya hayo".

Source: Bongo Movie
Zimeshapigwa hizo,hivi wachina na waNigeria nani tapeli zaidi,maana niliwahi kusikia waNigeria nao ni hatari kwenye hizo nyanja.?
 
Eti anahitaji msaada wa serikali.Kwani wakati wanakubaliana aliihusisha serikali?
 
Ni kama mil 84 mh... bongo movie inalipa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
HIVI WE WASTARA ULIPWE KABISA MILIONI 400 KWA MWAKA !

ahhahahahahhaa ni hizo picha za kifua wazi za bondi au kitu gani?
VITU VINGINE MUWAGE MNAJIULIZA!

sa na we kweli ukaona milioni 400 ,ukapiga mahesabu ukaona uweke zako 84!
AHHHHHAHAHAHHAHA ILA BONGO SIHAMI!
ACHA TU NIKOMAE NA FOLENI NA BEI YA UNGA!
ILA SIHAMI!
 
Apewe Mil. 400 kwa mwaka Wastara? vitu vingine tuwe tunajiongeza jamani...
 
Back
Top Bottom