Wastara alizwa mamilioni ya pesa na wachina

Wastara alizwa mamilioni ya pesa na wachina



Muigizaji maarufu wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ametapeliwa mamilioni ya fedha na kampuni moja ya simu ya Wachina baada ya kuingia nao mkataba wa kuwa balozi wao hapa nchini.
Wastara aliingia mkataba na Wachina hao mwaka jana ambapo alitakiwa awe analipwa shilingi milioni 400 kwa kila mwaka lakini ghafla Wachina hao wakaingia mitini.


“Pesa ambayo nawadai ni kama milioni 84. Kabla ya wao kuja nchini walitaka nianze kutumia pesa zangu kuandaa tisheti, kofia na mambo mengine ya kipromosheni. Kila nikiuliza kwamba mbona simu zenyewe haziji, maelezo yakawa kwamba wameagiza mzigo nje ya nchi, walipoona nawasumbua wakaingia mitini.

“Ilipopita miezi mitatu bila kuona maendeleo yoyote nilianza kuwasiliana nao tena, wakaanza kuniletea Kiswahili kingi, nikashtuka na kuweka mwanasheria wangu amba ambaye alikuwa nao sambamba, napo wakajaribu kumnyamazisha kwa pesa wakashindwa,” alisema Wastara.

Akaongeza kuwa, mara ya mwisho walikwenda kwenye kikao cha kujua hatima ya malipo yake na kinachoendelea ndipo afisa masoko wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Raymond Kalika alipomwambia kuwa Wachina hao wamerudi kwao.

“Yaani nahitaji msaada wa serikali ili nipate pesa zangu,hawawezi kunidhulumu kiasi chote hicho cha pesa katika kipindi kigumu kama hiki,” alisema Wastara.

Raymond ambaye ndiye aliyemuunganisha Wastara na Wachina hao alipoulizwa juu ya suala hili alijibu kwa kifupi:

“Ukweli wote nimeshamwambia Wastara, hapa tunasubiri hatua zifuatwe, siwezi kuwa na maongezi zaidi ya hayo".

Source: Bongo Movie
Huyo yuko location maisha yke ya kuungaunga tu aliolewa n sadifa ili apate matibabu hiyo 84m labda ya zimbabwe
 
Kwani serkal aliishirikisha mwanzoni kipind unapiga hizi dili zake? Na je ushuru kalpa?
 
Jamani hivi wastara nae kashakua brand ya kufikia kulipwa mil 400,mie warumi nilivyosikia niliguna tu maana mmh na yeye hajiongezi akili
 
Itakuwa Wachina walikuja kustuka kuwa walikosea kuchangua mhusika. Hii kazi angepata Wema ingezaa matunda.
Wema hana akili, deals ngapi kapata ila holla, labda jokate ,jide na vannesa wengine mamburula tu
 
Source bongo movie??

Huyu mdada hata kama hizo pesa kaongeza zero moja

Ila anamkosi aiseee,si ndio mlemavu wa mguu pia??

Daah wachina wale panya hawafai nawachukia balaaa
 
Source bongo movie??

Huyu mdada hata kama hizo pesa kaongeza zero moja

Ila anamkosi aiseee,si ndio mlemavu wa mguu pia??

Daah wachina wale panya hawafai nawachukia balaaa
 
Natumaini alisaini nao mikataba kazi hiyo na kiasi hicho cha fedha kiliandikwa humo na mengineyo pia.
 
Wema hana akili, deals ngapi kapata ila holla, labda jokate ,jide na vannesa wengine mamburula tu

Hao wengine sawa wana akili ila hawana bahati ukilinganisha na Wema.
 
Wasanii wa bongo muvi inabidi mjiongeze msipende vya bwerere
 
akili ndogo isije kutawala akili kubwa

ameona pa kutokea ndo hapo
 
Back
Top Bottom