miss confidence
JF-Expert Member
- Jul 9, 2016
- 393
- 273
Hiyo source yako sijui watu wanaochangia hawajaiona hahaaaaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo yuko location maisha yke ya kuungaunga tu aliolewa n sadifa ili apate matibabu hiyo 84m labda ya zimbabwe
Muigizaji maarufu wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ametapeliwa mamilioni ya fedha na kampuni moja ya simu ya Wachina baada ya kuingia nao mkataba wa kuwa balozi wao hapa nchini.
Wastara aliingia mkataba na Wachina hao mwaka jana ambapo alitakiwa awe analipwa shilingi milioni 400 kwa kila mwaka lakini ghafla Wachina hao wakaingia mitini.
“Pesa ambayo nawadai ni kama milioni 84. Kabla ya wao kuja nchini walitaka nianze kutumia pesa zangu kuandaa tisheti, kofia na mambo mengine ya kipromosheni. Kila nikiuliza kwamba mbona simu zenyewe haziji, maelezo yakawa kwamba wameagiza mzigo nje ya nchi, walipoona nawasumbua wakaingia mitini.
“Ilipopita miezi mitatu bila kuona maendeleo yoyote nilianza kuwasiliana nao tena, wakaanza kuniletea Kiswahili kingi, nikashtuka na kuweka mwanasheria wangu amba ambaye alikuwa nao sambamba, napo wakajaribu kumnyamazisha kwa pesa wakashindwa,” alisema Wastara.
Akaongeza kuwa, mara ya mwisho walikwenda kwenye kikao cha kujua hatima ya malipo yake na kinachoendelea ndipo afisa masoko wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Raymond Kalika alipomwambia kuwa Wachina hao wamerudi kwao.
“Yaani nahitaji msaada wa serikali ili nipate pesa zangu,hawawezi kunidhulumu kiasi chote hicho cha pesa katika kipindi kigumu kama hiki,” alisema Wastara.
Raymond ambaye ndiye aliyemuunganisha Wastara na Wachina hao alipoulizwa juu ya suala hili alijibu kwa kifupi:
“Ukweli wote nimeshamwambia Wastara, hapa tunasubiri hatua zifuatwe, siwezi kuwa na maongezi zaidi ya hayo".
Source: Bongo Movie
Kweli aseee............waleo ni chinapesaWachina wazuri ni wale waliojenga Tazara tuu. Hawa wa siku hizi ni [HASHTAG]#Wachinarapa[/HASHTAG]. # wachinaacademia
Wema hana akili, deals ngapi kapata ila holla, labda jokate ,jide na vannesa wengine mamburula tuItakuwa Wachina walikuja kustuka kuwa walikosea kuchangua mhusika. Hii kazi angepata Wema ingezaa matunda.
KzgSimu zinaitwaje?
Labda kiswahili cha kichina au uchina mwingi!Mi nimechoka hapo aliposema wachina walimletea kiswahili kingi. Mhn! Wachina wa wapi, Mbalizi?
ahahahaaaaaaa.....JF bhana raha kweliWachina wazuri ni wale waliojenga Tazara tuu. Hawa wa siku hizi ni [HASHTAG]#Wachinarapa[/HASHTAG]. # wachinaacademia
Kiswahili maana yake maneno ya ujanja ujanjaMi nimechoka hapo aliposema wachina walimletea kiswahili kingi. Mhn! Wachina wa wapi, Mbalizi?
Wema hana akili, deals ngapi kapata ila holla, labda jokate ,jide na vannesa wengine mamburula tu