Wasudan wajiuliza kuhamishwa raia wa nje kuachwa wao wapigane kuna hekima gani

Wasudan wajiuliza kuhamishwa raia wa nje kuachwa wao wapigane kuna hekima gani

Hao washenzi kutoka nje ndio chanzo cha chokochoko.Muda kama huu kama hao majenerali wanajua wanachopigania basi wangewashikilia mateka.Wakawaambia mutakufa pamoja nasi hapa.Mukileta ushoga na kuiba mali zetu mnataka uhuru lakini mambo yakiharibika munajali usalama wenu.
Umeandika nini mkuu
 
Mataifa karibu yote duniani yenye raia zao Sudan wanashindana kuwakimbiza nchini humo. Imekuwa kama ni siasa kuwahi kuwaondoa raia hao kwa mbinu tofauti. Nchi inayochelewa kufanya hivyo kama kwamba inahofia kuingia matatani kwa wananchi wake huko nyumbani.

Katika kuondoka huko kila nchi imekuwa ikifanya mbwembwe zake ili ionekane ni hodari zaidi katika kukimbia eneo lenye vita. Upande wa Marekani awali walisema wana mpanga wa kuwahamisha raia wake haraka. Kumbe wakati wakisema hivyo helikopta za Chinook zilikuwa tayari zipo Khartoum kuchukua maafisa wa ubalozi tu na familia zao wanaofikia 100.Wale raia wengine pacha wafikao 16000 kila mmoja ametakiwa aangalie usalama wake.

Uiengereza, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Spain na nchi nyingi zimeshafanya zoezi hilo. Kwa upande wa Urusi imesema raia wake wote wameshajikushanya ndani ya Ubalozi wa nchi hiyo Khartoum na wanaangalia muda muafaka ili kuwaondoa.Hali ni hiyo hata kwa vinchi vidogo kama Kenya na Misri nao eti wanafanya mipango kuondoa raia zao huo ambao huenda wala hawajui namna walivyoingia na wala idadi yao.

Majenerali wanaopigana nchini humo kila mmoja anajaribu kutoa picha kwamba ndiye aliyepanga mipango ya kusaidia kuondoka raia wa nchi moja baada ya nyengine. Kama wana madai ya kweli katika kuanzisha vita hivi basi badala ya kusaidia kuondoka raia hao wangewashikilia mateka mpaka usalama urudi nchini humo.Wangewaambia hawawezi kuwahakikishia usalalma wao.

Upande wa wananchi matukio hayo ya kukimbizwa kwa raia wa nje kumewakatisha tamaa sana.Alsadig Alfatih amesema kuwaona watu hao wakihamishwa na kuachwa wao wapigane kumemkatisha tamaa sana kwani alitaraji wao ndio wangesaidia kuleta amani.
6d24f0c0-e272-11ed-bffb-d0e242b79dbb.cf.webp
Hao majenerali unawashauri wawashikilie mateka raia wa kigeni kwa kigezo Cha usalama[emoji848]

Huwatakii mema hao na siku tu wanachuka huu ushauri wako ndio siku hiyohiyo ambayo watakuwa njiani kuungana na akina ghadafi.

Kiufupi tu hao majenerali hapo walipo wamezungukwa na mashushu wa hizo nchi za kikaburu so mipango yao ya kila siku taarifa zinafika kwa hao makaburu na wao ndio wanaoamua huo mgogoro uendelee au usiendelee na ukiendelea uchukuwe muda gani.

Ghadafi wkt anatoroka ndani ya comvoy yake kulikuwa na mole anayetoa taarifa ya njia zote anazopitia alipofika sehemu waitakayo ndio wakatia Moto msafara wake.

So kwa ushauri huo utawaharibia hao majenerali.
 
Muangalie huyu mwamba anayetajwa kuwa ndiye miongoni mwa walioongoza mauwaji huko Darfur kama ni kweli. jana ametoka jela baada ya jela kubomolewa. Anaitwa Ahmed Haroun. Kwa sura yake unaweza kusema ni kablila gani.
Jee huyu unawez kusema ndiye mwarabu aliyekuwa akiuwa waafrika huko Darfur. Katika machafuko kama haya wazungu wanapotaja ukabila wanajuwa wanachokifanya na faida zake.
230425230030-file-south-kordofan-ahmed-haroun.jpg
Kwani janjaweed si inafadhiliwa na waarabu wa sudani kina al bashir.
USA kawasaidia weusi wasiuwawe kwa kuwapa nchi yao.
 
Mshindwe kulinda amani yenu kazi kujazana ujinga tu, halafu mtegemee ngao wawe raia wa nje maajabu haya, acha wabaki mwenyewe ndiyo akili iwasogee, Trump aliwambiaje akili za mwafrika anaua raia wake wanaowatala, sijui anategea kutawala nini!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja tuangalie tujikumbushe.Lakini sidhani kuwa ilikuwa ni ushujaa wa Israel pekee iliambatana na ujinga wa vikosi vya Idi amin muda ule.Leo Israel hana ubavu huo tena
Usijidanganye hivyo, ukikosea mwenzio akashinda aliyeshinda ndiye shujaa.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Yaan waafrika bhn especially wabongo yaan Huwa hawajikubali kabisa et vinchi vidogo
 
Kama wanapenda wenyewe kupigana tuwasidianaje, kupigana ni tabia za wanyama, kama wameona kutumia nguvu ni muhimu kuliko akili, waache wapigane wakichoka watapatana.
 
Wamewachoka Sudani kusini Raisi na makamu wake walitwangana hasa mpaka baadaye akili ikawakaa sawa kumetulia

Sasa hivi ni zamu ya Sudani kaskazini Raisi na makamu wake wanatwangana akili zitawakaa sawa mbeleni

Sudani zote mbili Raisi huwa na jeshi lake na makamu huwa na lake sijui wana shida gani

Mataifa ya kiislamu mfano ya uarabuni hata siku moja waislamu waafrika nchi zenye waislamu watupu wakipigana iwe Somalia au Sudan,au libya,nk au popote huwa hawaingilii kati wala kutoa tamko la kulaani vita ila kwao ikilipuka kelele kila kona wanataka dunia iwaunge mkono

Waislamu wenzao uarabumi hawasaidii wanaondoa raia zao wanataka Marekani wakristo ndio wawasaidie?

Marekani alijaribu kuingia Somalia awasaidie kumaliza vita alishambuliwa na majeshi ya pande zote zinapigana kuwa hawataki mla nguruwe Somalia toka wewe,mmarekani, Marekani akakimbia akawaacha

Afghanistan vile vile akakimbia akawaacha waendelee kutwangana wenyewe huko mwislamu akimtwanga mwislamu mwenzie hadi kieleweke
Maajabu huanzia hapo, wanataka kafiri ndiye mtoa msaada, acha washikishane adabu ila wanao teseka wanawake na watoto jamani.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Let us call spade a spade vinginevyo Afrika hatutasonga mbele

Somalia wote waislamu mashehe wameenda kusuluhisha imeshindikana wanatwangana tu

Haya Sudan kaskazini hao wanatwangana sasa wote waislamu tena vita wameanza mwezi wa Ramadhan wasivyo hata na aibu dini moja hawaivi

Mifano iko kibao

Waislamu tumechoka na vita zenu za kutwangana wenyewe kwa wenyewe mnatia aibu bara letu la Afrika

Waambie na waislamu wenzao
Sasa hiyo nguzo alikuwa wanaitimiza vipi? Mchana kumwaga damu jioni kufuturu au!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe Urusi na Ukraine hawataki Suluhu kupitia DINI YAO MOJA ilihali mpaka baba mtakatifu ameingilia kati ila bado tu wanaendelea kuuana......

Unadhani dunia ya sasa watu wanapigania DINI na si FEDHA NA MADARAKA?!!!!

Kwenye baadhi ya nyumba za ibada tu za dini karibu zote mizozo,kutengana na kubaguana hakuishi kwa VIONGOZI sababu ya VISADAKA NA UKUU...sasa unashangaa kwa WANASIASA NA WANAJESHI HAO WAKUBWA wanaoshika HAZINA YA NCHI NA NJIA KUU ZA UCHUMI kisa tu wana majina ya kiislamu na ni waislamu?!!![emoji23]

Broad up your mind......

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Huko ni OTHODOX mzee, wala hawana fungamano na PAPA.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mataifa karibu yote duniani yenye raia zao Sudan wanashindana kuwakimbiza nchini humo. Imekuwa kama ni siasa kuwahi kuwaondoa raia hao kwa mbinu tofauti. Nchi inayochelewa kufanya hivyo kama kwamba inahofia kuingia matatani kwa wananchi wake huko nyumbani.

Katika kuondoka huko kila nchi imekuwa ikifanya mbwembwe zake ili ionekane ni hodari zaidi katika kukimbia eneo lenye vita. Upande wa Marekani awali walisema wana mpanga wa kuwahamisha raia wake haraka. Kumbe wakati wakisema hivyo helikopta za Chinook zilikuwa tayari zipo Khartoum kuchukua maafisa wa ubalozi tu na familia zao wanaofikia 100.Wale raia wengine pacha wafikao 16000 kila mmoja ametakiwa aangalie usalama wake.

Uiengereza, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Spain na nchi nyingi zimeshafanya zoezi hilo. Kwa upande wa Urusi imesema raia wake wote wameshajikushanya ndani ya Ubalozi wa nchi hiyo Khartoum na wanaangalia muda muafaka ili kuwaondoa.Hali ni hiyo hata kwa vinchi vidogo kama Kenya na Misri nao eti wanafanya mipango kuondoa raia zao huo ambao huenda wala hawajui namna walivyoingia na wala idadi yao.

Majenerali wanaopigana nchini humo kila mmoja anajaribu kutoa picha kwamba ndiye aliyepanga mipango ya kusaidia kuondoka raia wa nchi moja baada ya nyengine. Kama wana madai ya kweli katika kuanzisha vita hivi basi badala ya kusaidia kuondoka raia hao wangewashikilia mateka mpaka usalama urudi nchini humo.Wangewaambia hawawezi kuwahakikishia usalalma wao.

Upande wa wananchi matukio hayo ya kukimbizwa kwa raia wa nje kumewakatisha tamaa sana.Alsadig Alfatih amesema kuwaona watu hao wakihamishwa na kuachwa wao wapigane kumemkatisha tamaa sana kwani alitaraji wao ndio wangesaidia kuleta amani.
6d24f0c0-e272-11ed-bffb-d0e242b79dbb.cf.webp
Acha wapigane wenyewe wageni wote waondoke ana la wajitambue wapatane wajenge nchi yao....mafuta ni laana
 
Back
Top Bottom