Wasukuma hii ni karne ya 21 Tuelimike. Unasafirije na kuku kwenye basi kutoka mkoa huu hadi mkoa mwingine?

Wasukuma hii ni karne ya 21 Tuelimike. Unasafirije na kuku kwenye basi kutoka mkoa huu hadi mkoa mwingine?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Mimi ni mfugaji wa kuku,mbuzi na kwa uchache sana Ng'ombe hivyo huwa natambea maeneo na maeneo nakutana na kila aina ya mbegu za mifugo tajwa hapo juu.

Mara kadhaa nimekuwa nikishuhudia hii tabia ya kusafiri na kuku mara moja nimewahi safiri na msukuma na mbwa wa4 wadogo miaka na miaka bado hatubadiriki kabisa.Tunachosha angesema mgogo au mzaramo tungesema anatutania.

Sikatai kabisa kuwa kusafirisha mifugo tajwa hapo juu kuwa ni kosa lakini nakataa namna mifugo hiyo hasa kuku inavyosafirishwa kwenye gari la abiria.

Mtu anapanda gari mfano geita kwenda kahama ana vifaranga vya kuku 2 au kimoja ni kwamba huko kahama kabisa huwezi pata kifaranga cha sh 6000 hadi 10000 kama kweli wewe ni mdau wa ufugaji?

Mbaya zaidi unapanda na msukuma siti moja kutoka kahama hadi mpanda ana kuku wake ni safari ya siku nzima hii ni haki kweli?

Mambo mengine mnatufanya tuonekane wasukuma wote ni watu wasiojielewa mbaya zaidi ukiambiwa kwa lugha ya staha unajibu kwa sauti kuubwa halafu wasukuma wenzetu wasiojielewa kama wewe wanadikia utafikri umeomba lifti.

Wito kwa wenye magari angalieni namna nzuri za kusafirisha kuku sio tuwe tuna kaa na mtu aliyepakata kuku safari nzima akinya halufu yetu sote asee haifai

Hii ni kero

file_000000006ccc71fd982228c4c41b7ea3.png
 
Umenikumbusha kwenye treni jamaa alipanda na kuku, wale jamaa wa mle ndani walimsumbua Sana mshikaji wakamchukia yule kuku.

Tunafika mwisho wa safari eneo la jikoni tunaona manyoya tu yamezagaa.

Kwa ufupi Afrika ni shida, jamaa kupanda na kuku kwenye treni sidhani kama adhabu yake ilikuwa kuku wake kuchinjwa na kupikwa Supu.

Afrika Ustaarabu na kufuata Sheria bado Sana acha tuishi vile inawezekana
 
Kuna vitu vinaepukika mkuu. Halafu hili kabila letu hata awe amesoma vipi nina dada yangu ni Lecture chuo X mara kadhaa akija anabeba makuku kupeleka akafuge ukifika kwake huoni hata hao kuku alijisumbua kuwabeba unashangaa tu
 
Hawa jamaa wawe na magari yao maalumu kuwahamisha, maana hugeuka kero kwa abiri wengine. Ma special hire yawe yanawasafirisha wao na mifugo yao sio kusafirisha maiti tu na kwa wasukuma wahamaji wapelekewe magari hayo. Au hata malori ya kupakia mifugo ya wasukuma wanaohama yawepo, unakuta basi zuri ndani limechakaa, kunguni wamejaa sitini, huo si ni uchafu?
 
Back
Top Bottom