Wataalam, Msaada Tafadhali

Wataalam, Msaada Tafadhali

Kama imeomba unlock code, unahitaji IMEI number ya router yako:
Angalia chini ya router au andika *#06# ikiwa router ina skrini.Baada ya kupata unlock code, ingiza kwenye ukurasa wa kuingiza code (192.168.1.1) na bonyeza OK. Kama ni sahihi, router yako itakuwa unlocked na itaweza kutumia laini yoyote.
 
Naomba nisaidie mkuu. Nipe maelekezo tafadhali. Nitakupa soda mkuu
Weka SIM kadi mpya kutoka kwa mtoa huduma tofauti kwenye router yako.

Washa router na uunganishe na kifaa chako kupitia Wi-Fi au USB.

Fungua link na uende kwenye anwani ya router (kawaida 192.168.1.1 au 192.168.8.1).

Ingia kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri (kawaida ni "admin" kwa zote mbili). Utaombwa kuingiza code wa kufungua. Ingiza code uliopata na uhakikishe.
 
Back
Top Bottom