Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
unataka kuamia kwenye fani ya upishi mdogo wangu?habari ya siku ya leo wapendwa wana JF, naombeni mnisaidie kutafsiri maneno yafuatayo kwa lugha ya kiswahili maana nimehangaika kutafuta tafsiri yake bila mafanikio yoyote.
- Recipes
- Cuisines
- Main Dish
- Side Dish
- Appetizers
Maneno hayo yanayo onekana hapo juu hutumika sana kwenye mambo ya vyakula sasa usije ukaona dish hapo juu ukaniambia ukatafsiri vingine.
unataka kuamia kwenye fani ya upishi mdogo wangu?
Mie nagusia maeneo matatu; Ukitaka neno moja tu linaloshikilia maana ya maneno umetoa then kazi ipo! 🙂
Recipes ni simply viungo vinavyotumika kwenye mapishi, kama vile nazi, pili pili, binzari, n.k
Cuisines naweza sema kuwa ni "Pishi la kitamaduni" sababu ni aina ya vyakula kwa misingi ya tamaduni/eneo Fulani. Unaweza kuwa na cuisine ya Kihaya, Kichagga, Kinyakyusa or whatever tegemeana na taratibu la hilo kabila ama eneo.
Appetizers naweza sema kama "Vitia hamu" kama kuna mwingine ana neno zuri zaidi atujuze. Mara nyingi hutumika katika chakula kumfanya mtu kujisikia kula chakula kwa hamu zaidi.
Hiyo ya tano ni chachandu
Recipe-viungo
cuisine- Kuremba tu, jibu ni msosi
Main dish- dishi kubwa eg Dstv
Side Dish-Dish la pembeni eg Star times
Appetizers-Hatuna hili neno kwa kiswahili maana tunazaliwa na "Appetite' kubwa sana kutoka kwa mtengenezaji
safi sana, nina uhakika siku tutakayokutembelea/utakayotutembelea tutafaidi sana mapishi yako......Mbona nimeshahamia siku nyingi dada yangu...huna habari?
Hiyo ya tano ni chachandu
Hiyo ya tano ni chachandu
safi sana, nina uhakika siku tutakayokutembelea/utakayotutembelea tutafaidi sana mapishi yako......
Naam, umetafsiri vyema dada yangu AshaDii lakini mimi nilikuwa nahitaji kupata tafsiri ya hayo maneno kwa lugha ya kiswahili kwa neno moja tu. Mfano: Breakfast - Kifungua Kinywa.
Chachandu ni shanga zile za machangu bana.
Naam, umetafsiri vyema dada yangu AshaDii lakini mimi nilikuwa nahitaji kupata tafsiri ya hayo maneno kwa lugha ya kiswahili kwa neno moja tu. Mfano: Breakfast - Kifungua Kinywa.
Cuisine-Mapishi
Recipe- Viungo
Main Dish-Mlo Halisi
Side Dish-Mlo Nyongeza
Appetizer-Kileta Hamu
Ku brainstorm raha
Ndiyo maana nilitanguliza kuwa kama unataka neno moja tu lazima italeta shida. Ukiyapata tafadhali nishtue... Na naomba nikukumbushe kuwa hata huo mfano hauna tofauti na tafsiri zangu. Kama vile Appetizer nilivyosema ni "Vitia hamu" ndivyo Breakfast ilivyo na "kifungua kinywa"
Umenote kuwa hakuna tofauti?
That is to say ukaamua kutumia neno moja la Chachandu (alilotuwasilishia CalvinPower ) kuwa ndiyo utumie kwa neno "Appetizer" inakuwa bado ina mapungufu sababu Chachandu ni Appetizer... Ila si Appetizer zote ni Chachandu.
Kwenye recipe - viungo hapo ntapingana na wewe kwa sababu ndani ya recipe huwa kuna vitu vifuatavyo;
- Appetizers
- Beverages
- Breakfasts
- Desserts
- Lunch
- Main Dishes
- Side Dishes
Sasa unataka kuniambia hivyo navyo ni viungo?