Wataalam wa telecom nini maana ya alama hizi E H+ 3G & 4G kwenye simu?

Wataalam wa telecom nini maana ya alama hizi E H+ 3G & 4G kwenye simu?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Nimekuwa nikiona hizi alama zikijitokeza mara kwa mara kwa mpishano kwenye simu yangu ila sijajua zina maana gani.

Na je zinavyobadilika haziathiri ubora wa huduma kwa thamani ya fedha niliyolipa?

Wajuzi tieni neno kidogo hapa.
 
E-Edge,H-HSDPA,3G-3rd Generation,4G-4th generation.Tofauti halo Ni Speed
 
E == 2G (Japo naweza kutokua sahihi).

3G== Hii inajieleza Network speed yake sio kubwa kivile, at least kwa hapa Bongo, so ki ujumla ni hovyo tu nayo.

H na H+==Bado ni 3G ila ni advanced sana, Hapo ndo unyama una anza hapo kama H imetulia iko moto sana, b+inafsi 4G ukiyumbaga hua naforce i stay kwenye H).

4G== Hii ndo unyama kabisa, speed ni nzuri ila ni kutegemea na maeneo pia na mtandao husika.
 
Nimekuwa nikiona hizi alama zikijitokeza mara kwa mara kwa mpishano kwenye simu yangu ila sijajua zina maana gani.

Na je zinavyobadilika haziathiri ubora wa huduma kwa thamani ya fedha niliyolipa?

Wajuzi tieni neno kidogo hapa.
Network ya 2G kuna G (GPRS) na E (EDGE) E ni more advanced na inaspeed kubwa kuliko G
H (HSPA) na H+ (HSPA plus) ni 3G. H+ ni more advanced na inaspeed kuiliko H
Hizo ni generation tofauti za Cellular Network (Cellular network ndo hii unayoiona inagaiwa kwa minara)
Zamani mtandao ulikuwa unagaiwa kwa cable, so ukitaka kuunganisha kifaa chako utavuta cable, ikaja ya wireless lakini nyingi ilikuwa kila mtu analewa fixed channel yake ikawa shida apo kuwa na watumiaji wengi
Mpaka miaka ya tisini kama sikosei ndo wakaja na hii cellular technology, hapa unagawa eneo kubwa kwenye vijumba tunaviita cells halafu kila kijumba kinakuwa na mnara (cellular tower) ambao unachannel kadhaa kwa watumiaji kadhaa. Hala ilianzaga generation ya 1 ya cellular 1G,ikaja 2G (hii ndo ilikuja na vitu kama sms, data (GPRS then EDGE)) etc), tukaja na 3G (generation ya tatu), tukaja ya 4,tukaja ya 5 na saivi inaenda 6G
Hizi generation zinatofautiana capacity(how many channels) , data rate (speed) nk
 
Nimekuwa nikiona hizi alama zikijitokeza mara kwa mara kwa mpishano kwenye simu yangu ila sijajua zina maana gani.

Na je zinavyobadilika haziathiri ubora wa huduma kwa thamani ya fedha niliyolipa?

Wajuzi tieni neno kidogo hapa.
Umesahau UMTS, WCDMA, TDMA, CDMA/CDMA2000.
Japo ulitakiwa kuanza na google, lakini HSPA speed ni up to 21Mbps na HSPDA 41Mbps++ anyway goodlucky
 
Back
Top Bottom