Baadhi ya Wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wamelalamikia kuwepo kwa wataalam wachache wa kipimo cha CT-Scan kunahatarisha usalama wa wagonjwa wao.
Wananchi hao wamesema mara kadhaa wanapofika hospitalini hapo wagonjwa wamekuwa wakichukua muda mrefu kupata matibabu huku wakiambiwa kuwa mtaalamu yupo mmoja na mara kadhaa anakuwa hayupo kabisa lakini wamesema hiyo inaweza ikawa hatari kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka.
Wananchi wameendelea kuhoji je, endapo kuna ajali imetokea inayohitaji kipimo hicho je nini hatma ya wagonjwa hao.
Wameomba Serikali kuangalia upya huduma za CT-Scan katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
============
Updates...
Akijibu hoja hiyo, Kaimu Afisa Uhusiano wa Umma wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro, Scholastica Ndunga amesema “Sio kweli, tuna wateja wachache kuliko uhalisia, kwa siku wakizidi sana ni watano, imefikia hatua Mkuu wa Idara ametuagiza kwenda Wilayani kutangaza ili wateja waongezeke.”