Macbook pro
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 722
- 1,030
Habari zenu wakuu!?
Natuamini mko pouwa kama unaumwa au una smongo wa mawazo basi polee mkuu, yanamuda tu yatakuwa poua.
Niende kwenye maada. Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya ambapo kwa kuona na kusikia nimekumbana nao. Nianze na haya maeneo ambayo kiukweli ni janga kubwa!
Wataalamu wa Tehama. (IT)
Kuna siku nikiwa nafanya kazi kama kujitolea katika hospitali fulani mkoani Arusha, kulitokea hitilafu ya mfumo wa Kuendesha na kutunza Kumbukumbu za huduma za afya zinazotolewa kituoni hapo. Tukamjulisha IT juu ya changamoto hiyo, jamaa ni mnene likitanbi hilooo, jamaa akaja akachungulia akasema ngoja nitakuja baadae nirekebishe ile baadae mwamba akarudi baada ya kurudi jamaa kaanza kufungua browser na kuanza kusearch ...How to troubleshoot ...... ! Mbele yetu na jamaa jasho likawa linamtoka kabisa. Na huyu mwamba ana Shahada ya Computer science. Akaendelea kuangalia mara akakutana na video ya mhindi mmoja anaelezea namna kutibu hilo tatizo. Jamaa akafunga browser akarudi kwenye system akajaribu wapii. Baadae ikabidi ampigie jamaa mmoja ni freelancer ana office yake hapo Mjini jamaa alipokuja akaingia kwenye system akafanya kama nusu saa hivi mambo yakarudi. Yeye jamaa mwenye likitambi lake akampatia jamaa hela ya maji kwa sababu wanajuana na kama washikaji wanajuana. Muna mwingine huku Halmashauri nilipo huyu IT anachojua ni kuelekeza namna ya kufungua Akaunti ya GOTHOMIS ila ikitokea error yoyote hajui. Anaitwa IT, mmh sasa hizi shahada na stashahada mlipataje wakuu au ndio ajira za kupeana tu. Ovyooo sana.
Kada ya Afya
Kuna njemba mmoja nilikuwa nafanya nayo kazi, Huyu ni mfamasia bhana. Huyu mwamba ni Aibu, utasikia mimi ni mfamasia blah blah ilaukija kwenye shule yupo empty anachojua nikuingiza dawa na vifaa tiba kwenye ledger kazi ambayo hata mtu aliyesoma procurement anaweza kuifanya. Na ukienda kuulizia matumizi ya Dawa ikiwemo na madhara yake kwa wafamasia waliopo mtaani wanajua vitu ila hizi njema huku kwenye mfumo hamna. Nawaza tu kwanini inakua hivi ?
Maafisa Biashara.
Hawa jamaa wanachojua ni kukutolea control number ya Leseni na service levy ila kukushauri namna ambavyo ungefanya ili ku boost biashara yako ili waweze kukusanya mapato bila kipengele hamna. Yaani mijamaa inachojua ni kutengeneza control number. Wazee, hebu zitumieni shule zenu kusaidia wafanya biashara au hamuna kitu kwa kuchwa mnachojua ni kutoa control number na kufungia maduka kama hajalipia service levy au leseni.
Walimu 😄
Hawa jamaa bhana asee, mbinu za ufunidishaji sijui wamesahau au lah. Walimu walioko kwenye shule za private wanafundisha sana na kwa mbinu ambazo kuna muda nawaza hivi walimu walioko privatewalisoma Cuba na walioko huku kwenye kidumu na mfagio ndio waliosoma kwenye vyuo vyetu. Mjitafakari. Mtoto hadi anafika darasa la tano hajui hesabu vizuri na hata kusoma ni kwa shida ila mwalimu hata hajigusi. Wakati mtoto huyo huyo ukimpeleka private akiwa darasa la kwanza anakua anajua mambo mengi. Ni nini shida ?
Wakadarasi nao mule mule. 😆
Wakandarasi jamii na wakandarasi wa majengo walioko kwenye Halmashauri daah ni masikitiko asee. Kila siku kwenye maredio wanalalamikiwa kwa kusimamia ujenzi ambao majengo yake yana ubora wa chini wakati mwingine kuna watu wanaswekwa ndani. Lakini wakandarasi walioko kwenye makampuni bianfsi ni tofauti. Ishu ni nini wakuu?
Shida ni nini ? Mifumo ya usaili au mifumo ya elimu yetu inakasoro mahala fulani ?