vitus juma
Member
- May 20, 2015
- 98
- 43
Mara nyingi nikilala muda wa usiku hasa saa kumi na moja kuna kitu hunijia na kukaa mwilini kiasi kwamba huwa nashindwa kupumua, kuna wakati huwa kikinikalia huwa nasikia kikitoa pumzi, siyo hapo tuu pia kitu hicho kinaponijia huwa mwili wangu unatetemeka na ninaposhituka huacha kisha hurudi tena na tena mpaka kihakikishe kimenibana pumzi.
Mara nyingi huniletea ndoto za kutisha kinachonishangaza ni kuwa muda mwingine huwa nakuwa macho na huwa ninapumua kama kawaida ila uwezo wakugeuka au kutingishika au kuongea huwa nakosa. Hivi sasa ni mwaka wa saba toka tatizo lianze na toka limenijia ni zaid ya mara 2000 kwani kuna kipindi hufululiza hata kwa week mara 4 napenda nijue hili tatizo ni nini? Ni uchawi, jinamizi au ni nini? Na suluhisho lake ni nini?
Karibuni