Wataalamu, hiki ni nini?

Wataalamu, hiki ni nini?

vitus juma

Member
Joined
May 20, 2015
Posts
98
Reaction score
43
Mara nyingi nikilala muda wa usiku hasa saa kumi na moja kuna kitu hunijia na kukaa mwilini kiasi kwamba huwa nashindwa kupumua, kuna wakati huwa kikinikalia huwa nasikia kikitoa pumzi, siyo hapo tuu pia kitu hicho kinaponijia huwa mwili wangu unatetemeka na ninaposhituka huacha kisha hurudi tena na tena mpaka kihakikishe kimenibana pumzi.

Mara nyingi huniletea ndoto za kutisha kinachonishangaza ni kuwa muda mwingine huwa nakuwa macho na huwa ninapumua kama kawaida ila uwezo wakugeuka au kutingishika au kuongea huwa nakosa. Hivi sasa ni mwaka wa saba toka tatizo lianze na toka limenijia ni zaid ya mara 2000 kwani kuna kipindi hufululiza hata kwa week mara 4 napenda nijue hili tatizo ni nini? Ni uchawi, jinamizi au ni nini? Na suluhisho lake ni nini?

Karibuni
 
Usiende kulala tumbo zikiwa zimeshiba sana.
Angalau panda kitandani baada ya lisaa limoja baada ya kula au saana 45 dk.
 
Hiyo hata mie hunitokea pale ninapolala late hours. Nakumbuka kipindi nasoma ndio ilikuwa kero .nadhani kuna jambo hapo linalitokana na ubongo kuchoka maana hata wewe umesema inatokea ukilala muda umeenda. Kipindi nasoma nilianza mpaka kuogopa kusoma usiku
 
Last edited by a moderator:
Jaribu kulala kwenye mazingira masafi, Ili upate hewa safi na ubongo ufikirie mema. Safi chumba, acha kusonyeka nguo chafu, na pia uwe unaoga. Usiku kula, usilale na njaa.
 
mkuu #smart911 nakuomba upitie lmaelezo haya hapo chini;
The nervous system includes the central nervous system (CNS), which consists of the brain and the spinal cord, and the peripheral nervous system (PNS), which is all the nerves outside of the central nervous system which connect it to all parts of the body. The peripheral nervous system is further divided into two branches: the somatic and autonomic nervous systems (ANS). The somatic nervous system is composed of the motor system which has outflowing nerves that control the movements of the muscles and the incoming sensory nerves which transmit messages from the body to the CNS. The autonomic nervous system controls all the involuntary processes of the body which function largely below the level of consciousness such as heart rate, digestion, respiration, perspiration, urination, and sexual arousal. Although some actions such as breathing, work in tandem with the conscious mind.
kimsingi tatizo lenyewe linaitwa kwa kimombo NIGHTMARE ama kwa kikwetu ni JINAMIZI
Hutokea hasa pale mtu anapokuwa amesinzia usingizi wa fo fo fo
ama usingizi wa pono ,
hii inatokea pale ambapo mfumo wa (autonomic nervous system) unakuwa chini ya kiwango cha kuweza kuendesha matendo yasiyo ya hiari kama vile heart rate , digestion, respiration kwa kutaja vichache vinavyotuhusu, huo mfumo wa nerve ukiwa chini ya kiwango hupelekea oksijeni inapungua katika ubongo hivyo mhusika anahisi kama anakabwa
hiyo haina uchawi ni matokeo ya huo mfumo wa ANS Kuwa chini ya kiwango chake na kufanya ubongo kupungukiwa na oksijeni,:sleepy::yawn:

Mimi nina tatizo usiku nasikia masikio yanaimba nilienda kwa dr wa ENT muhimbili akaniambia kuna hitilafu kati ya system ya hewa inayopitia masikioni je kuna ukweli
 
Mara nyingi nikilala muda wa usiku hasa saa kumi na moja kuna kitu hunijia na kukaa mwilini kiasi kwamba huwa nashindwa kupumua, kuna wakati huwa kikinikalia huwa nasikia kikitoa pumzi, siyo hapo tuu pia kitu hicho kinaponijia huwa mwili wangu unatetemeka na ninaposhituka huacha kisha hurudi tena na tena mpaka kihakikishe kimenibana pumzi.

Mara nyingi huniletea ndoto za kutisha kinachonishangaza ni kuwa muda mwingine huwa nakuwa macho na huwa ninapumua kama kawaida ila uwezo wakugeuka au kutingishika au kuongea huwa nakosa. Hivi sasa ni mwaka wa saba toka tatizo lianze na toka limenijia ni zaid ya mara 2000 kwani kuna kipindi hufululiza hata kwa week mara 4 napenda nijue hili tatizo ni nini? Ni uchawi, jinamizi au ni nini? Na suluhisho lake ni nini?

Karibuni[/QUOTE
Kaombewe,,DELIVERENCE[kuhudumiwa ] kwa jina la YESU KRISTO na baada ya hapo kama utapenda kwenda hospitali nenda ufumbuzi utapatikana.
 
Mkuu huyo ni jinamizi.
Anawatokea watu wengi tu WANAOLALA CHALI. Nadhani hata wewe ni shuhuda wa hilo! {kwamba mara zote alizokutokea ni ktk hali ya mlalo huo}

Dawa ni kutolala chali.
Ikiwa huwezi jaribu kulala na jani la mmavi mavi mfukoni.
 
Back
Top Bottom